Habari wanajamii,
Aisee nimekuja kuweka kero yangu hapa nikitumaini pengine mamlaka husika zitaona na kuangalia namna ya kutatua changamoto hii.
Nianze kwa kupongeza Serikali na mamlaka husika namna zinajitahidi kupunguza madhara yatokanayo na ajali za barabarani hususani kwa mabus. Siku hizi tunaona ajali bado zipo ila madhara ikiwemo idadi ya vifo etc ni kidogo kulinganisha na zamani hii ikimaanisha initiatives mbalimbali zilizowekwa zinafanya kazi. Initiatives hizo ni pamoja na kuweka ving'amuzi kwenye mabus, tochi, askari barabarani n.k.
Binafsi naamini kama initiatives hizo zikisimamiwa vizuri pengine kutakuwa ni suluhisho la kudumu ila pia naona kuna hili suala la timetable ambalo naona ni kero sana kwa abiria na sioni kama lina mantiki katika kuzuia mabus kukimbia. Hii ni kero kubwa hasa kwa mikoa ya nyanda za juu Kusini. Unakuta ratiba inasema kutoka Dsm, inabidi kufika stand ya Iringa, Igumbilo saa 7.30 mchana, sasa najiuliza kama tayari kuna tochi na ving'amuzi kwenye mabus ambavyo vina monitor speed ya chombo ili kitembee mwendo elekezi (80-85kph) kwanini bado unamwambia afike sehemu flan mda flan?.. Kwamba akiwahi inabidi asubiri sehemu hadi mda elekezi ufike! Hii inasababisha usumbufu na uchovu usio na lazima kwa abiria kwa kujikuta mnasimama sehemu karibia saa nzima ili tu kusubiri mda.
Hii naona sio sawa, badala yake mamlaka zingejikita katika kuhakikisha kuna ufanisi wa ving'amuzi, tochi nk. ikiwemo maoperator huko LATRA ili mabus yatembee mwendo elekezi mwanzo mwisho. Kuwepo na adhabu kali kisheria dhidi ya either operator ama askari wataoonekana "kula michongo" ili mabus/ kampuni flan yakimbie zaidi ya speed elekezi. Naomba mamlaka zifanyie kazi hili ama zitafute namna ya kutuondolea kero ya kusimama sehemu bila shughuli yeyote ili kusubiri timetable. Naomba kuwasilisha.