ngoshwe
JF-Expert Member
- Mar 31, 2009
- 4,131
- 937
Nafanya kazi, laki tisa KITU NI mshahara wangu wa mwezi unasoma kwenye "salary slip" lakini kiasi nachoingiziwa benki ni laki nne na USHEE tu. Hii inatokana na makato kibao, nakatwa bima ya afya (27, 565.20) , malipo ya bodi ya mikopo ya vyuo vikuu (18,377.08), mfuko pensheni, (45,942) , mkopo mdogo niliokopa benki (ZAIDI YA 200,000). Kodi ya mapato (163,882).
Inaonekana kodi kwa kuajiriwa ni klubwa sana. Miaka fulani serikali ilifuta kodi ya kichwa na baadae ushuru kwa mazao ya kilimo ili kuwaondolea kero wakulima (wananchi). Lakini cha kusikitisha nchi hii kufanya kazi imekuwa kero, tupu, ukiwa unafanya kazi na wakati huo huo ni mkulima na mfanyabiashara nadahani utayaona maumivu ya hizi kodi.
Sisi tulioajiriwa hatulalamiki sana tunapokatwa " pay as you earn (paye)" ambayo wajanja wachache wanaitumia kuishi japo ilitarajiwa kuwasaidia wengi lakini bado hao wengi ndio imekuwa mzigo kwetu, tuna ishi nao majumbani tukitumia nao hicho hicho kidogo tunachopokea baada ya kukatwa !.
Kule ulaya na marekani, wale wanaoishi kwa kutegemea posho na uwezeshaji wa umma ( "ma-benefit" ) wengi wameamua ni heri wasifanye kazi kabisa ili waendeelee kuhudumiwa na serikali kuliko kufanya kazi halafu ukaishia kupokea mshahara kichele baada ya makatio kibao.
SINA HAKIKA KAMA HIVI VYAMA VYETU VYA WAFANYAKAZI VINAJUA MAJUKUMU YAKE VIZURI..SISI WANYONGE TUNAUMIA. NI HERI SERIKALI INGEAMUA KUANDIKISHA KILA FAMILIA NA KUJUA MAHITAJI YAO NA IKIWEZEKANA IKAANZISHA UTARATIBU WA KUZIHUDUMIA ZILE AMBAZO HAZINA UWEZO..UNAKUTA KATIKA FAMILIA NYINGI ZA KITANZANIA PENGINE MTU MMOJA TU NDIE ANAEFANYA KAZI LAKINI ANAWAJIBIKA KULISHA NA KUTOA HUDUMA ZA JAMIII KWA KAYA ZAIDI YA TATU ZENYE WATU WASIOPUNGUA KUMI KATIKA KILA KAYA (MTU MMOJA ANAHUDUMIA FAMILIA YAKE YA MKE/MUME NA WATOTO, ANAHUDUMIA PIA FAMILIYA YA WAZAZI WAKE, WAKWE ZAKE NA ANAWAJIBIKA PIA KUTOA MICHANGO YA MAENDELEO YA JAMII IKIWEMO HARUSI, NK...) HALI HII INAWAFANYA WATANZANIA WENGI WAISHI MAISHA MAFUPI KUTOKANA NA MARADHI YANAYOWAPATA WAKIWA BADO VIJANA....NA HATA WAKIENDA KUTAFUTA HUDUMA ZA AFYA, KILE WANACHOKATWA HAKIONEKANI KUPELEKWA HUKO ILI KIWASAIDIE KUWATIBU..