KERO za TRA Iringa

Mlyafinono

Senior Member
Joined
Apr 6, 2012
Posts
177
Reaction score
47
Hizi ni miongoni mwa kero za TRA iringa.

unakwenda katika ofisi husika kwaajili ya huduma fulani.

unapewa account ukalipie bank, unarudi na risiti ya bank kuonyesha umeshalipia, lakini chaajabu hupati huduma ati kwasababu pesa hiyo hawaioni kwenye mtandano wao.Unaweza ukasota wiki nzima unafuatilia huduma ambayo umeshalipia lakini kwasababu hawaioni kwenye mtandao wao licha ya kuwa na risiti ya bank huwezi kupewa huduma hiyo.

Jambo lingine ni mtandao mbovu wa internet.Kila ukienda mara mtandao umekata, kero hizi hadi lini.Inamaana pamoja na kukusanya kodi zote hizo hawajaunganishwa kwenye mkongo wa taifa?.

Huu siyo uungwana jamani
 
Naipenda sana Tanganyika! Hebu irudisheni tuachane na hilikitu linaitwa Tanzania! Limeoza! Hao wanataka tu rushwa. Nenda TAKUKURU, waeleze kinachoendelea kisha wekeni mtego. La sivyo utasumbuliwa mpaka basi....!
 

Wewe haujajua tu ukitaka uwakuhudumie toa kadi ya magamba, kitu fasta ushahudumiwa . kulewa sifa eti NAFANYA KAZI T-R-A , ntalipeleka mamlaka fulani nyeti ili tuweke mtego wa kuwatia nguvuni watu kama hao wanaohachafua sifa ya ofisi. I AM GOING TO DEAL WITH THEM PERPENDICULARLY
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…