Kero za TRA mkoa wa Iringa

Kero za TRA mkoa wa Iringa

towashi wa kushi

JF-Expert Member
Joined
May 15, 2024
Posts
332
Reaction score
729
Kumekuwa na kero nyingi toka kwa TRA mkoa wa Iringa zinazooelekea migomo ya wafanyabiashara wa bidhaa mbalimbali na hata sisi wafanyabiashara wa mbao tuna mgomo.

Zifuatazo ni kero tunazokumbana nazo wafanyabiashara wa mkoa wa Iringa (Wilaya zote 3 za Mufindi, Kilolo na Iringa)

1. Kubambikiziwa madeni ya miaka iliyopita na kufungiwa akaunti zetu. Leo Wafanyabiashara wa Manispaa ya Iringa wamefunga maduka leo Mei 31, 2024 kwa zaidi ya saa nne wakiilalamikia Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) kwa kuwapa na kuwabambikizia madeni ya zaidi ya miaka mitano iliyopita na kuwatolewa lugha ya vitisho wanapokwenda kuhakiki makadirio ya biashara zao sambamba na baadhi yao kufungiwa akaunti zao za fedha.

2. Kulazimishwa kwa wafanyabiashara na wakulima wa mbao kununua mashine za EFD.
Sisi wafanyabiashara wa mbao tuna mgomo wiki ya pili sasa kwani tunalazimishwa kununua mashine za EFD ili tuweze kusafirisha mbao zetu. Pamoja na hayo, sisi wafanyabiashara tukiwa na mashine za EDD, bado tunatakiwa tuoneshe risiti za EFD toka kwa wakulima wa miti ya Mbao.

Ukienda kwa wakulima wanaotuuzia mbao, wanatakiwa wawe na mashine za EFD ili watuuzie siso mbao. Kuna vitu vinashangaza na kusikitisha sana sasa nchini. Yaani mkulima mwenye miti 5 au 10 baye anatakiwa awe na mashine ya EFD ili anapotuuzia mbao atupe risiti ambazo nasi tunatakiwa tuwaoneshe TRA lasivyo wanataka tuwape rushwa.

3. Kufungiwa kwa biashara zetu kwa kisingizio cha kulazimishwa kuwa na mashine ya EFD pindi Mfanyakazi wa TRA anapotaka kufungua biashara kama yangu. Hii imetokea kwa wafanyabiashara wa dry cleaner kule Kilolo na wafanyabiashara wa Pembejeo kwani Meneja away TRA wilaya alitaka na akafungua dry cleaner yake so akalazimisha competitor wake kufunga biashara. Pia Mufindi, Meneja anataka kufungua duka la mbolea sasa analazimisha wafanyabiashara wa mbolea kuwa na efd wakati huo huo wakikadiliwa pesa nyingi za kodi ili washindwe kufanya biashara

Kwa hiki, kinachoendelea serikali kuu ingilieni kati kwani tunanyanyasika sana wafanyabiashara wa Iringa ndani ya nchi yetu.

1717149465811.jpg

Hali ya mgomo wa wafanyabiashara ilivyokuwa leo hapa Iringa Mjini.
 
View attachment 3004687
Hali ya mgomo wa wafanyabiashara ilivyokuwa leo hapa Iringa Mjini.
Tulipe kodi
 
Back
Top Bottom