Kero za WhatsApp

Group likiwa limepooza
 
MIMI NI CCM DAMU-----MIMI NI YANGA DAMU-----MIMI NI TANZANIA DAMU----MIMI NI TEAM MAGUFULI DAMU---- MIMI NASEMA KWA KAULI MOJA "MITANO TENA, KAZI IANZE"
too much sauce!! umesoma heading vizur au mihemko ya chama chako ndio inakupeleka puta?
 
Kulazimishana kuchati... kuna kipindi kwenye group la o level, watu tusiopenda kuchati tuliwekwa kitimoto tukawa tunasimangwa eti kwa nini tunasoma chats tu bila kuchati. Baada ya kikao hicho wajumbe wakakubaliana watuleftishe....basi ikawa hivyo. Binafsi nikasema eeephhhhh
 
Group la biashara watu wanaleta mambo ya siasa.
Group la siasa watu wanaleta mambo ya mapenzi.
Group la mapenzi watu wanaleta mambo ya ujenzi.
Group la ujenzi watu wanaleta mambo ya soka/kubeti.
Group la msiba watu wanaleta utani [emoji204]
 
Kuingizwa kwenye group bila kuombwa ridhaa binafsi , unajistukia umedumbukizwa hujui group ya nini inahusiana na nini.

Wewe admin mfate mtu privately , omba ridhaa yake ya kumuunga..
 
Ni kero zipi unakumbana nazo kwenye magroup mbalimbali ya WhatsApp uliyopo Hadi unatamani ku left.
Wale wanaotuma link za bofya hapa upate free 250 GB kwenye groups wanakera sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…