Mie huwa inachukuwa hata miaka miwili au mitatu sometimes kupanda daladala. Sababu kuu ni kwamba muda mwingi siko mjini. Ila inapotokea nakuwa mjini wakati wa kuchukua dalala inanijia kumwuuliza kondakta nauli ni shilingi ngapi. Kuna konda wazuri wanakujibu pila matusi. Ila kuna wengine sasa.... majibu utakayopata utajuta kuuliza nauli kiasi gani. Na baadhi ya abiria wengine kwenye daladala wanaona kama unajidai. Kumbe hata. Nauli huwa sina badilika kila nikija mjini. Halafu vituo saa nyingine navyo vinabadilika.