Kesho kuna Maandamano ya Wafanyakazi kudai Sheria ya Mafao Ibatilishwe

MPadmire

JF-Expert Member
Joined
Mar 7, 2006
Posts
3,957
Reaction score
3,245
Ndio, muda huu nimesikia kwa BBC kuwa kesho kuna maandamano.
 
wanaandamania uingereza?

Ngoja nikatafute mabomu ya machozi proof.
 
Upuuzi huu, nani alisema maandamano huleta tofauti yeyote Tanzania? Jikomboeni kwanza kutoka utumwa wa akili, mkaache woga wa kijinga na mkiisha kupata ujasiri nendeni mkaandamane. Kwa Tanzania hii, itapita miaka 200 hadi wananchi kudevelop moyo wa ujasiri na kuandamana kwa nia moja. Otherwise upuuzi tu huu, mi siandamani.

Kassanga.
Tabora.
 

Wewe ndio kikwazo cha mabadiliko
 

Huna haja ya kutoa povu lote hili for the sake of just saying huandamani.Mabadiliko ya kifikra kwa sasa yanatia moyo.Kuandamana hata kama ni kwa kuungaunga it shows that now we are at least starting to dare.
 
Mkuu maandamano ya Wafanyakazi kudai haki yao wewe inakuathiri vp?
 
Jamani yataanzia wapi hayo maandamano.kama ni kesho mi niko tayari wadau
 
Itakuchukuwa muda mrefu sana kuelewa maana ya post yangu, soma kwa maarifa ugundue nini kilichomo katikati ya mistari yangu. Usikurupuke kujibu post zangu utabaki njia panda kamanda, fungua akili ya ziada acha papara; penye nguvu hutoka mlo lakini penye uchungu asali hujisokota. Alamski.
Wewe ndio kikwazo cha mabadiliko
 
hawawezi kukuelewa ndugu yangu,sisi tuliokunywa sifongo ndo tunaweza kukuelewa tu!nisalimie huko tbr maeneo ya mwinyi, bhachu,isevya,chemchem,bila kusahau cheyo kuna siku nitarudi tbr nitakutafuta mkuu labda tunaweza kupata pa kuanzia
 
Kasanga,unapoweka post unatarajia watu waelewe bt unapoweka ili watu wasielewe mi nakuona km tatzo...ww kaa nyumbani upike mkeo akaandamane!Solidarity forever!
 
Jamni mwenye details atuambie hayo maandamano yanaanzia wapi hadi wapi? Yana kibali au hayana? ili watu tuwe tayari kwa lolote.
 
Uko sawa kabisa, maandamano bila Plan B ni sawa na li-upepo-litavuma litapita litasahaulika.
 

maandamano haya ni ya wafanyaka wala hayakuhusu wee mkulima wa Tabora, we nenda shamba ukalime matobolwa
 

mwanaharakati achana naye mkulima huyo wa Tbr
 
hawawezi kukuelewa ndugu yangu,sisi tuliokunywa sifongo ndo tunaweza kukuelewa tu!nisalimie huko tbr maeneo ya mwinyi, bhachu,isevya,chemchem,bila kusahau cheyo kuna siku nitarudi tbr nitakutafuta mkuu labda tunaweza kupata pa kuanzia
mkulima mwenzie mkulima bora mkale sifongo zenu huko Tbr. Na kama ni wafanyakazi basi mtakuwa wa kazi za ndani, hamuwekewi akiba
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…