SoC02 Kesho yangu ni kesho kuu

Stories of Change - 2022 Competition

Simulizi za Shafih

New Member
Joined
Aug 27, 2022
Posts
2
Reaction score
0
KESHO YANGU NI KESHO KUU.

Mwandishi Simulizi za Shafih.

Baada ya jogoo wa kwanza kuwika nilijinyanyua kitandani na kukaa kitako. Siku ile jogoo hakuniamsha usingizini Bali alinifanya nijue kuwa kumekwisha pambazuka.

"Sasa nijiandae Kwa safari ya kibaruani"nilijisemea wakati nateremka kitandani.

Kwa majina naitwa Cholo Kwa wakati ule nilikua naishi peke yangu baada ya wazazi wangu kufariki. Kifo Cha wazazi wangu kilinirudisha sana nyuma kwani ile ajali ya moto iliyotokea pale nyumbani iliteketeza Mali zote na kufanya niishi maisha ya kutanga tanga.

"Hapana natakiwa nisimame kama mwanaume, nisimame kama mtu mwingine alivyosimama na kuweza kufanikiwa" nilikua najisemea mara kadhaa kila nilipohisi kukata tamaa.

Ukiwa huna chochote basi wale watu wako wote wakaribu hukukimbia na unaweza kusaidiwa na mtu ambae hata hukumtegemea,

"Oyaa vipi Samwel?"nilisalimia baada ya simu kupokelewa.

"Samwel hayupo katoka" Kwa mbali nilisikia sauti ya kike ikinipa taarifa ile lakini ilinipa wasiwasi kwani sauti ile ilikua inatokea katikati ya mdundo mkubwa wa muziki.

"Huyu atakua disco na huyu aliyepokea simu ni mwanamke wake"niliongea mwenyewe huku nikiamini kuwa hata ile ilikua ni namna tu ya rafiki zangu kunitelekeza.

Upweke ulizidi kunizonga huku nikijaribu kuwaza wapi nianzie. Hakukua na chaguo lingine zaidi ya kujiingiza katika kazi ya kuosha magari. Japo sikuwa na uzoefu wowote lakini nikiamini kuwa nina uwezo wa kufanikiwa kupitia kazi ile.

Upande wangu ilikua ni ngumu kuaminiwa mpaka nipewe kazi huku baadhi yao wakihisi nimekuja kuwatania au kuchunguza jambo Fulani, lakini hata wale waliokuwa marafiki zangu walizidi kunitenga huku wakinicheka zaidi.

"Hahahaha!! Mwana kayumba saana yaani. Hivi unaweza kuamini kuwa Cholo amekua chura" aliongea Samwel akiwa ameshika glass ya mvinyo huku mwanamke akiwa amemkalia mapajani.

"Aaah acha utani bwana yaani chura vipi una maanisha"aliuliza Fred.

"Jamaa kazi yake ni kuosha magari sasa hivi yaani juzi nimekutana nae mwamba kachakaa kaisha mpaka nikamwonea huruma" aliongea Samwel. Hayo yalikua maongezi Yao mara nyingi wanapokutana. Haikuwa kawaida wao kuachia kuzungumza kuhusu mimi.

"Huwez kuwa na Mimi tena, Mimi sio wa kutembea na vibaka waosha magari naomba ukome kuniita ita majina yako ya ajabu na ukome kunifuata, nikiona unafanya tena huu upuuzi wako nitakuitia mwizi kibaka mkubwa wewe" aliongea Regina ambae alikua mpenzi wangu.

"Kuwanini unanifanyia hivyo Regina naomba rudisha moyo wako nyuma naomba kumbuka tulipotoka mimi na wewe, mangapi tulofanya mimi na wewe leo unaniita mimi kibaka kwasababu tu ya hali yangu ya uchumi imebadilika. Naomba utambue kuwa maisha ni hatua leo nimesimama katika jua kesho labda nitakua nimesimama kivulini."nilimwambia huku akiwa anachezea ufunguo wa gari ndogo aliyokua amekuja nayo.

"Wewe lalamika tu njaa lakini ujue tu Kuna vidume mjini wanajua kugharamia na kutumia sio wewe kibaka muosha magari" aliniambia na kuondoka.

Katika maneno yote hakuna neno lililoniumiza kama kuniita mimi kibaka, nilitaka siku moja nimwonyeshe namna Gani kibaka nimekua, sikuwahi kukata tamaa kabisa kwani niliamini kuwa kesho ndio siku ambayo hakuna anaejua itakuaje.

Katika kazi yangu nilijitahidi sana kubana matumizi huku nikiwa makini sana kazini.
"Natakiwa kujifunza udereva kupitia kazi yangu ili niweze kutimiza ndoto zangu.

"Kama naomba unisogezee hii gari pale niikaushe" nilimwomba kijana ambae tulikua tunafanya nae kazi anisaidie kuendesha gari mpaka sehemu nzuri.
"Ujitahidi na wewe ujue gari bwana sio Kila siku unaomba tu tusipokuwepo atakae kusogezea ni nani" aliniambia maneno yale yaliyonifanya nijisikie vibaya lakini sikukata tamaa kwani niliamini Kuna siku na Mimi jitaweza.

***********
Ndani ya miezi mitatu nilikua nimeshakuwa dereva mzuri sana na sasa nilikua nahangaika kutafuta leseni yangu ili niweze kuomba kazi katika mashirika makubwa makubwa.

Kupata leseni haikuwa ngumu kwani nilipata msaada wa kishoka.
" Naona unatembea na bahasha mkononi kaka ushaanza kuwa tapeli nini? Aliniambia Fred siku moja tulipokua tumekutana katika mihangaiko.

"Ah hamna kaka ni kupambana tu na haya maisha si unajua Mimi Sina kitu lazima nipambane"nilimwambia.

"Okay poa Mimi Niko hapo ndani casino "aliongea na kuondoka.
Hali yangu iliniweka mbali na rafiki zangu.

Baada ya wiki mbili nilipata kazi katika kampuni ya usafirishaji.

Mazingira ya kazi yalikua mazuri sana baada ya mwaka nilikua nna viwanja viwili huku nikiendelea na ujenzi.

Sikuwahi kukata tamaa ndio maana Leo hii Niko hapa. Rafiki zangu Fred, Samwel huwa wananipigia simu kunipongeza.

MWISHO
 
Upvote 1
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…