Wakati zimebaki siku mbili kupiga kura ninachukua fursa hii kuomba Watanzania wenzangu kujitokeza kwa wingi kwenda kutimiza wajibu wetu wa kitaifa. Tumesikia ajenda na ahadi za wagombea mbalimbali ni jukumu letu kupima na kufanya uamuzi ulio sahihi kwa kuangalia mahitaji ya nchi.
Maneno matamu yamesemwa lakini ni bora kuyatafakari kwa kina. Haya nayasema kama mzalendo kwa leo bila kumshawishi mtu aegemee upande fulani lakini watanzania ni watu wenye hekima na busara watachagua kulingana na mizania hususani ikizingatiwa kuwa sote tunapiga kura tukiwa na miaka si chini ya 18 umri wa mtu mzima mwenye maamuzi.
Aidha, tujiepushe na fujo na kuvunja Sheria za nchi wakati na baada ya uchaguzi. Na wataoshindwa wakubali matokeo na iwapo hawataridhika wafuate sheria za rufaa.
Kwa haya machache ninawatakia Uchaguzi mwema.
Mtumishi wa umma Mwandamizi Mstaafu.