Kesi dhidi ya Lwakatare: Ndivyo TISS hufanya kazi? Kupeleka kwanza ushahidi muhimu mtandaoni?

Kesi dhidi ya Lwakatare: Ndivyo TISS hufanya kazi? Kupeleka kwanza ushahidi muhimu mtandaoni?

Zak Malang

JF-Expert Member
Joined
Dec 30, 2008
Posts
5,404
Reaction score
239

Nina tatizo kubwa sana na hili sakata la video ya Lwakatare na video yake. Mwenye ufafanuzi/maelezo ya kina atujuze hapa:

Kuna mtazamo mwingine wa hili sakata la video ya Lwakatare, mtazamo ambao nasdhindwa kuunganisha dots.. Naomba msaada

1. Kuna thread moja iliwekwa jana ikionyesha akina Michuzi wakipongezana kutokana na Usalama wa Taifa (TISS) ‘kuleta kitu hiki' na kwamba ni ‘kete kubwa kwetu' – bila shaka kete kubwa dhidi ya Chadema. Katika thread hiyo kulizuka tatizo la kutafsiri (yaani kulikuwapo ambiguity) kuhusu maneno (intepretation) ya pongezi hizo kwa TISS ni kwa ajili ya nini hasa – yaani kwa jitihada halali za TISS kuchunguza na hatimaye kupatikana hiyo video; au pongezi zililenga kwa wao TISS ‘kuipika' hiyo videoa kwa ajili ya kubambikizia CDM?
2. Sasa hata tuchukue hiyo tafsiri ya kwanza – kwamba TISS ndiyo walifanikisha kuchunguza na kupatikana hiyo video ambayo bila shaka itakuwa ni ‘ushahidi' mkubwa wa kesi dhidi ya Lwakatare na pengine CDM pia, jee hii ndiyo njia sahihi kwa TISS, au tuseme ndiyo utaratibu wao wa kuuweka kwanza ushahidi huu muhimu mtandaoni kabla ya sualakupelekwa mahakamani? Nasema hivi iwapo video hiyo ni kutokana na jitihada zao za halali wenyewe TISS yaani wao ndiyo exclusive owner wa hiyo video kama jinsi akina Michuzi walitaka sis tuamini. Inakuwaje waitumbukize kwanza mtandaoni? Ndivy utaratibu siku hizi?
3. Kwa nini TISS wasingekaa nayo kimya kimya tu halafu kuishtukizia mahakamani baada ya kumkamata Lwakatare? Ushahidi mkuu wa kesi unawekwa bayana kwa jamii kwa njia ya mtandaoni kabla ya kesi kuanza?
4. Lakini pengine TISS hawakuwa mmiliki pekee (exclusive owner) ya video hiyo yaani nao waliipata kutoka kwingine (labda from Mchemba?) lakini hata hivyo haikuwa sahihi kitaaluma za mambo ya upelelezi na mashitaka kuiweka kwanza mitandaoni – kwa lengo gani?
5. Na ndiyo sasa nakuja na tatizo langu kubwa kuhusu sakata zima hili: Yeyote yule (TISS au Mchemba) waliiweka video kwanza mtandaoni ili kupima joto ku-test waters) kuhusu uhalisia wake) na wameona kwamba video hiyo imejikuta inatobolewa matundu mengi tu (punched holes) hadi uhalisia wake kuonekana wa mashaka. Kweli TISS hufanya kazi kwa mtindo huu?
6. Mie nadhani ni Mchemba (aliyewahi kutangaza huko nyuma kwamba anayo video ‘inayoonyesha viongozi wa Chadema wakipanga mauaji' lakini baadaye akajikuta video ina mapugufu mengi kuhusu alichokitangaza na ndiyo maana badala ya kuipeleka polisi (kama jinsi akina Dr Slaa walivyomtaka kuipeleka), au kuwapa TISS wai-deal nayo -- aliona ni vyema aiweke mtandaoni. Na sababu kubwa kufanya hivi ni kwamba iwapo itaonekana ni video ni bomu (yaani ya kughushi), basi isijulikane kama ni yeye ndiyo aliiweka mtandaoni na hivyo kukwepa lawama. Na ndiyo maana kumetokea ugumu wa kumpeleka Lwakatare mahakamani kwa haraka.
7. Video hiyo haimuunganishi moja kwa moja Lwakatare kuhusu kupigwa kwa Kibanda hivyo bila shaka waliokuwa nayo waliishikilia kwanza (was put on hold) hadi "tukio la Kibanda" litokee ndiyo ikawekwa mtandaoni. Hii bila shaka ilitakiwa jamii iwekwe kwanza kisaikolojia kuhusu yatakayofuata."
8. Na yaliyofuata sasa tumeyaona – watu walipangwa ku-act nafasi zao kama ilivyotakiwa (according to the laid down script). Hawa wengine ni pamoja na Manyerere -- na hata huyo Ludovick na tukio lake lile la kutekwa ili kujitafutia alibi. Nahisi Ludovick atakuwa shahidi tu wa kujaribu kuakandamiza viongozi wengine wa CDM – ingawa hawatajwi katika video.
Mimi naona mpango mzima uliosukwa umekwenda kombo mahali fulani. Bado tISS wanakosa uweledi wa kufanya operations zao – kuanzia tukio la kuuwawa kwa Gen Amrani Kombe, Chacha Wangwe, tukio la tindikali la Kubenea, kutekwa kwa Ulimboka na pengine hili la kupigwa kwa Kibanda.

Naomba tujadili hili kwa kina.

Hakuna kesi hapo ni kuchezea hovyo kodi zetu,alafu wanabwagwa Mahakamani.
 
Analysis hii ndio inayozunguka kichwani mwangu na ninahisi hii ilipangwa iwe series ambapo wangekuja na part nyingine, kama ingefanikiwa na bado wangewaleta na wengineo ambao ni tishio kwa CCM in the same way kama hii ingefanikiwa lakini God aitwe Mungu, Allah hakika ashukuriwe daima kawaumbua kweupe tena bila kuhitaji utalaamu mkubwa au wakuazima from outside.
Kwanini mnatuchelewesha wa TZ kufika nchi ya ahadi?? Unadhani hatutamani mafanikio ya Rwanda?? Au hii nchi ni mali ya kina Mwiguli, NIpe na Rizmoja na jmaa zao?? But this time no mm nitajitolea kuelimisha na kubadili mioyo ya wachache kuelewa nimeanza na my family and friends wote somo limewaingia, wamelewa ubaya wa CCM na vibaraka wao kina Mnyerere, Mjngwa na Michzi. Mungu wape nguvu watetezi na wapiganaji wote mpk kieleweke.
 
mtazungusha maneno kwa sana tu, amerekodiwa na vijana wenu wenyewe, moja imeenda TISS na nyingine imeenda youtube.
 
Ninapata ugumu sana ninaposikia Mwigullu alipata first class UDSM na anafanya upumbavu kama huu na mwingine mwingi - pia anaweza kupata vyeo na kutumia fedha za walipa kodi. Najiuliza hao wasomi huko nyumbani Tanzania wakoje na wanauwezo gani? Samahani sana ndugu zangu ila ninatatizwa sana na elimu yenu hapo nyumbani ingawa nashukuru Mungu watoto wangu siyo sehemu ya Taifa la wajinga - (Tanzania). Wenzetu wa Rwanda wanawaza maendeleo sisi tunapika mikanda ya Lwakatare hivi watanzania wenzangu mlioko nyumbani mna akili kweli????
 
nasali sana mungu azidi kuwaumbua. Maana mungu anasema usimshuhudie jirani yako uongo.
 
Analysis hii ndio inayozunguka kichwani mwangu na ninahisi hii ilipangwa iwe series ambapo wangekuja na part nyingine, kama ingefanikiwa na bado wangewaleta na wengineo ambao ni tishio kwa CCM in the same way kama hii ingefanikiwa lakini God aitwe Mungu, Allah hakika ashukuriwe daima kawaumbua kweupe tena bila kuhitaji utalaamu mkubwa au wakuazima from outside.
Kwanini mnatuchelewesha wa TZ kufika nchi ya ahadi?? Unadhani hatutamani mafanikio ya Rwanda?? Au hii nchi ni mali ya kina Mwiguli, NIpe na Rizmoja na jmaa zao?? But this time no mm nitajitolea kuelimisha na kubadili mioyo ya wachache kuelewa nimeanza na my family and friends wote somo limewaingia, wamelewa ubaya wa CCM na vibaraka wao kina Mnyerere, Mjngwa na Michzi. Mungu wape nguvu watetezi na wapiganaji wote mpk kieleweke.

Mkuu hii strategy ya kuellimisha Familia au ukoo ikitumiwa vizurii nadhani ni nzuri!
 
Hard Hitter;
Umechambua vzr, na nadhan uchambuz huu utawasaidia weng kuona utata wa video ile.
Ingawa tunaonekana tunamtetea Lwakatare, lakn kama kila mtu akituliza akil yake vzr na kukusanya matukio na kaul za viongoz (Utawala), utagundua utata mkubwa sana.

MASWAL NI MENGI KULIKO MAJIBU;
>Nan ameiweka video mtandaon?
>Aliipata lin?
>Kwanin hakuipeleka polis?
>Kwann imetolewa baada ya Kibanda kuteswa, tukio ambalo polis wanahusishwa.?
>Vp kuhusu ukimya wa Nchemba, Wasira na TISS ambao mara kadhaa wamekuwa wakijitokeza haraka kujibu tuhuma zinazowakabil mitandaön & magazetn, kwann wako kimya kuhusu hil?
>Je tuna iman na jesh la polis, kuchunguza swala hili hasa kiteknolojia? Je wapo huru kiutendaji?
>Kuna uadui mkubwa kias gan kat ya waandish na Lwakatare ama Chadema? Na ni kwa matukio yapi?
>Kwann hapelekw Mahakaman mpaka leo, tatizo ni nin kama kwel kila kitu kipo waz (Video)??

CONCL; NI SIASA NA PROPAGANDA ZA WATAWALA (CCM) KUWAZIMA UPINZAN NA WAANDISH WA HABARI NCHIN.

WANANCH NDO WAAMUZ WAKUU, kusuka ama kunyoa.
 
Ninapata ugumu sana ninaposikia Mwigullu alipata first class UDSM na anafanya upumbavu kama huu na mwingine mwingi - pia anaweza kupata vyeo na kutumia fedha za walipa kodi. Najiuliza hao wasomi huko nyumbani Tanzania wakoje na wanauwezo gani? Samahani sana ndugu zangu ila ninatatizwa sana na elimu yenu hapo nyumbani ingawa nashukuru Mungu watoto wangu siyo sehemu ya Taifa la wajinga - (Tanzania). Wenzetu wa Rwanda wanawaza maendeleo sisi tunapika mikanda ya Lwakatare hivi watanzania wenzangu mlioko nyumbani mna akili kweli????

Maneno makal sana kijana, nadhan ingekuwa vema ungemlenga huyo huyo uliyemtaja kuliko kujumuisha wote (Nchi). Au ni dharau tu na kujidai kuwa umefika huko? Kwan wee ulisomea wap kabla ya kufika huko?

Rudin nyumban 2015 kupiga kura, kama kwel mnataka mabadiliko, sio maneno tu.
 
Ninapata ugumu sana ninaposikia Mwigullu alipata first class UDSM na anafanya upumbavu kama huu na mwingine mwingi - pia anaweza kupata vyeo na kutumia fedha za walipa kodi. Najiuliza hao wasomi huko nyumbani Tanzania wakoje na wanauwezo gani? Samahani sana ndugu zangu ila ninatatizwa sana na elimu yenu hapo nyumbani ingawa nashukuru Mungu watoto wangu siyo sehemu ya Taifa la wajinga - (Tanzania). Wenzetu wa Rwanda wanawaza maendeleo sisi tunapika mikanda ya Lwakatare hivi watanzania wenzangu mlioko nyumbani mna akili kweli????
Omuregi wasu wenye akili hapa Tanzania wamebaki kule kwenu kisiwani Ukara tu.Sehemu nyingine wote ni kama Mwigulu Nchemba.Hebu fikiria first class economists wa Tanzania ni aina ya Mwigulu je hayo madaraja mengine wakoje?.Dunia inawaza jinsi ya kupambana na changamoto za kiuchumi lakini kwetu wachumi wanaandaa mipango ya kuwaangamiza Watanzania wengine tena kwa njia za kipuuzi kama hizi.
 
Hard hitler umeweka vyema kabisa,kuna watu hapa jukwaani waliwahi kuhoji kazi za TISS sasa hapa tumeelewa vizuri lakini kwa issue ya Lwakatare wameshaangukia pua,naona kwa mwendo huu watawatokomeza kabisa magamba,yetu macho.
 
Hata Mimi nimejiuliza sana, ethics za upelelezi zinasemaje?
 
Hhi movie ya lwakatare haina shule yo yote hata chembe. Wasomi hawafanyi upuuzi kama huo.
 
Ndio maana JK aliomba FBI kuja kufanya upelelezi wa mauaji ya Padri kule zanzibar coz anajua hii TISS yake haijui chochote, ona aibu inayowakumba hata kum-frame LWAKATARE wameshindwa, sijui walitumia software gani kufanya hiyo kazi, vegas au adobe premiere......TISS ya Nyerere haitakaa irudi katika zama hizi za utawala wa CCM kwa staili yao kuingizana huko as if wanaingizana kwenye Club ya CCM.
 
watafute ushahidi mwingine huo video ya kutengeneza hauwezi kumtia mtu hatiani....hili zao la 4/4 lipo toka zamani
 
mtazungusha maneno kwa sana tu, amerekodiwa na vijana wenu wenyewe, moja imeenda TISS na nyingine imeenda youtube.

kuna njama za mauaji zinazofanyika bar kama siyo kuishiwa sera? Mbona hizi zinazofanywa na serikali ya ccm kupitia TISS haziitaji hata king'amuzi kujua ni njie mmetekeleza hayo?
 
Ninapata ugumu sana ninaposikia Mwigullu alipata first class UDSM na anafanya upumbavu kama huu na mwingine mwingi - pia anaweza kupata vyeo na kutumia fedha za walipa kodi. Najiuliza hao wasomi huko nyumbani Tanzania wakoje na wanauwezo gani? Samahani sana ndugu zangu ila ninatatizwa sana na elimu yenu hapo nyumbani ingawa nashukuru Mungu watoto wangu siyo sehemu ya Taifa la wajinga - (Tanzania). Wenzetu wa Rwanda wanawaza maendeleo sisi tunapika mikanda ya Lwakatare hivi watanzania wenzangu mlioko nyumbani mna akili kweli????

Mkuu elimu ya huku kwetu haimpimi mtu kuelewa bali kujariri na hata wengi walio na vyeti wengine siyo vya kukaa darasani bali hata rushwa na kuchonga, kwahiyo hiyo farst class yake inawezekana kapitia njia za kiccm
 
Back
Top Bottom