Kesi inayomkabili Mwalimu wa Shule ya Green Acres anayedaiwa kumlawiti mtoto yaahirishwa hadi Machi 24, 2025

Kesi inayomkabili Mwalimu wa Shule ya Green Acres anayedaiwa kumlawiti mtoto yaahirishwa hadi Machi 24, 2025

Nyakijooga

JF-Expert Member
Joined
Dec 9, 2018
Posts
276
Reaction score
473
Kesi Namba Cc 32444/24 inayomkabili Saleh Ayoub (39) mkazi wa Salasala Dar es Salaam, Mwalimu wa Shule ya Msingi Green Acres iliyopo Mbezi-Africana anayedaiwa kumlawiti Mwanafunzi imetajwa Februari 26, 2025 lakini imeahirishwa kutokana na sababu iliyoelezwa, kwamba Afisa ambaye alitakiwa kumuandaa shahidi alipata udhuru.

Akizungumza Mahakamani hapo, Wakili wa Jamhuri ameiambia Mahakama kwamba walikuwa na shahidi mmoja ambaye alitakiwa kutoa ushahidi wake, lakini amedai kuwa Afisa wa Mahakama ambaye alitakiwa kumuandaa shahidi huyo amepata udhuru hivyo kushindwa kutekeleza ukamilifu zoezi hilo.

Kufuatia sababu hiyo Wakili wa Jamhuri aliomba Mahakama kuahirisha kesi hiyo ili kupangiwa siku nyingine.

Aidha, kwa kuzingatia rika ya shahidi aliyetakiwa kutoa ushahidi wake upande wa utetezi umekubali sababu hiyo.

Baada ya kuwasilisha sababu hiyo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Hawa Magesa, kesi hiyo imeahirishwa mpaka Machi 24, 2025 ambapo itakuja kwa ajili ya kutajwa.

Itakumbukwa Jamhuri ilieleza kwamba katika kesi hiyo watakuwa na mashahidi sita na kielelezo kimoja, ambapo mpaka sasa shahidi mmoja ndiye ametoa ushahidi wake.

Kwa mara ya kwanza mshtakiwa huyo alipandishwa kizimbani muda mfupi baada ya Mwanachama wa Jamiiforums.com kuhoji sababu za kutofikishwa mahakamani kwa watuhumiwa aliodai wanahusika na vitendo vya ukatili katika Shule ya Green Acres iliyopo Mbezi Africana Jijini Dar es Salaam.

Hata hivyo, baada mshtakiwa kufikishwa Mahakamani alisomewa shtaka la ulawiti lakini alikana kuhusika.

Kusoma ilipotoka kesi hii, soma:
~
Watu 6 kutoa ushahidi Kesi ya Mwalimu wa Shule ya Green Acres anayetuhumiwa kumlawiti Mwanafunzi wake

~ Dar: Mwalimu wa Shule ya Green Acres anayedaiwa kumlawiti Mwanafunzi wake afikishwa Mahakamani

~ Walimu wa Shule ya Green Acres (Dar) wanaotuhumiwa kulawiti na kuwadhalilisha Wanafunzi, wanalindwa na nani?

~ Kesi ya Mwalimu wa Shule ya Msingi Green Acres anayetuhumiwa kulawiti Mwanafunzi yaahirishwa Mwezi mzima, Hakimu apata hudhuru

~ Watu 6 kutoa ushahidi Kesi ya Mwalimu wa Shule ya Green Acres anayetuhumiwa kumlawiti Mwanafunzi wake

~ Ushahidi wa Kesi ya Shule ya Msingi Green Acres, Saleh Ayoub anayetuhumiwa kumlawiti Mwanafunzi wake kuanza kutolewa Februari 6, 2025
 
Back
Top Bottom