Kesi inayoongoza kwa kusikilizwa na kuisha kwa muda mfupi

Llio 002

JF-Expert Member
Joined
Jul 14, 2015
Posts
1,636
Reaction score
2,053
Kuna kesi moja ilikwenda Mahakama ya Mwanzo huko Tanga. Kijana wa miaka 20 alikuwa anataka kupewa mgao wake wa mali za marehemu baba yake.

Ni kweli alikuwa na mgao wake, ila mjane wa marehemu alikuwa anamuona bado mdogo kuweza kumiliki mali. Marehemu alikuwa ameacha magari na nyumba kadhaa.

Basi yule kijana baada ya kuona mama hataki kumpa mgao wake akafungua kesi mahakamani.

Kufika mahakamani kijana kaulizwa, "Unamtambua huyu?"

Akajibu, "Ndiyo. Ni mama yangu mzazi."

Na mama akaulizwa, "Unamtambua huyu?"

Mama akajibu, "Ni mwanangu wa kumzaa."

Kijana akaambiwa, "Eleza mahakama madai yako ni yepi?"

Kijana akajibu, "Madai yangu ni nikabidhiwe mgao wangu wa mali za marehemu baba. Mama nimemwambia amegoma kunipa."

Mama akaulizwa, "Unasemaje kuhusu hayo madai?"

Mama akajibu, "Huyu ni mwanangu wa kumzaa, ila sikumzaa na huyo aliyeacha hizo mali."

Kesi ikaishia hapo hapo.
 
Hakukuwa na Wosia boss vile vile dogo hakulitegemea hilo swali mahakamaninso akawa hana cha kuongeza au kuuliza tena
Kesi haiwezi kuisha kimzaha namna hiyo.

Kuna hoja ya kujadili hapa.

Kama huyo kijana aliandikwa kwenye wosia wa mgao wa mirathi, hata angelizaliwa na baba mwingine, mgao wake unamhusu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sio tatizo marehemu alikuwa ni mlezi tu, ila kiuhalisia ni kweli dogo alizaliwa na marehemu ila bimkubwa aliamuwa kumfanyia makusudi tu
Ila kisheria anatambulika ni mtoto wake na ana ubini wake
 
Sio tatizo marehemu alikuwa ni mlezi tu... ila kiuhalisia ni kweli dogo alizaliwa na marehemu ila bimkubwa aliamuwa kumfanyia makusudi tu
Kisheria ni mtoto wake, hata kama alikuwa adopted, mlezi hampi ubini anaemlea, analuwa mlezi tu, ukimpa ubini kisheria ni wako.
 
Hakuna cha kuthibitisha mkuu kama marehemu alimtambua huyo mtoto kama wake,mama ndio anajuwa kila kitu kuhusu mtoto anaweza kusema tu kuwa baba yake mzazi huyu mtoto alifariki akiwa mtoto bado ndio marehemu huyu wa sasa akaamuwa kumlea tu kama wa kwake
Marehemu alimtbua huyo kama mtoto wake, hata kama alikua adopted
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ