Kesi inayoongoza kwa kusikilizwa na kuisha kwa muda mfupi

Kuna kesi moja ilikwenda Mahakama ya Mwanzo huko Tanga. Kijana wa miaka 20 alikuwa anataka kupewa mgao wake wa mali za marehemu baba yake.

Ni kweli alikuwa na mgao wake, ila mjane wa marehemu alikuwa anamuona bado mdogo kuweza kumiliki mali. Marehemu alikuwa ameacha magari na nyumba kadhaa.

Basi yule kijana baada ya kuona mama hataki kumpa mgao wake akafungua kesi mahakamani.

Kufika mahakamani kijana kaulizwa, "Unamtambua huyu?"

Akajibu, "Ndiyo. Ni mama yangu mzazi."

Na mama akaulizwa, "Unamtambua huyu?"

Mama akajibu, "Ni mwanangu wa kumzaa."

Kijana akaambiwa, "Eleza mahakama madai yako ni yepi?"

Kijana akajibu, "Madai yangu ni nikabidhiwe mgao wangu wa mali za marehemu baba. Mama nimemwambia amegoma kunipa."

Mama akaulizwa, "Unasemaje kuhusu hayo madai?"

Mama akajibu, "Huyu ni mwanangu wa kumzaa, ila sikumzaa na huyo aliyeacha hizo mali."

Kesi ikaishia hapo hapo.[emoji16][emoji16]
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787]Ni balaa
 
Judgement ilimalizwa na mama mzazi [emoji3][emoji3]
Hakuna kitu kama hiko Mkuu,hizi stori huwa nazikataa zinalengo la kufurahisha tu.Haina tofauti na ile jamaa alikamatwa na bang baada ya kwenda mahakama akakubali ila akasema bangi yake ilikuwa gunia bas polisi aliyemkamata akafungwa hapo hapo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…