Kesi na hukumu ya vigogo Zantel na Halotel inanuka rushwa!

Kesi na hukumu ya vigogo Zantel na Halotel inanuka rushwa!

Taso

JF-Expert Member
Joined
Jun 12, 2010
Posts
2,507
Reaction score
2,412
1. Imekua kuaje ndani ya siku 20 vigogo wa Telecoms waliokamatwa na kukutwa na hatia ya uhujumu uchumi wa zaidi ya bilioni moja, tena serial offenders (Halotel, kila siku wanakamatwa) wameachiwa huru kwa kulipishwa fine ya mil 200 ambayo ni chini ya robo ya walichoiba, bil 1.1?

2. Kwa nini DPP alitaka kesi iendeshwa Kisutu badala ya Mahakama Kuu kama sheria inavyosema kwa kesi zote za uhujumu uchumi?

3. Kuna watu wako mahabusu miaka 5 kwa kesi za uhujumu uchumi za kiasi kidogo kuliko hawa... hawa wamekamatwa, wamekuwa arraigned, wameshitakiwa, wamechunguzwa, kesi imeendeshwa, wamekutwa na hatia, wamehukumiwa, ndani ya siku 20, wamelipa kiasi gani cha kuuweka mfukoni mfumo wa mahakama hawa watu?

4. Hivi ni kwa nini Muafrika huwa anajinyima haki yeye mwenyewe halafu anatetemeka mbele ya "mzungu" hata wa Vietnam na Egypt, anampa chochote anachotaka ilhali halafu tunaambiwa na Rais tembeeni vifua mbele?

halotel-zantel-jpeg.800046


Kuna Watanzania wenzetu walianzisha kikampuni chao cha telecom (Rashid Shamte, Dr. Ringo Tenga, Peter Noni, Noel Chacha n.k.) wanaoza mahabusu mwaka wa pili sasa kwa kesi ya kutoa huduma chini ya bei elekezi, hawa sio binadamu mbele ya hao "wazungu" wa Vietnam na Egypt walioachiwa?

Source:Matukio yaliyotokea kipindi JamiiForums ilipokuwa haipo hewani
 
Babu yangu siku zote aliniambia "Hatima ya kuku aijua Mfugaji"
 
Mwenye njaa hakatai chakula akikataa ujue kapata pilau la sikukuu atakula baadae.
 
Back
Top Bottom