Jaji ameingia..
Kesi inatajwa...
Quorum zipo vile vile...
Mtobesya: Shahidi Wakati Mnamkamata Ling'wenya ni taarifa zipi Mlikuwa nazo tayari?
Shahidi: Taarifa tulizokuwa nazo alikuwa ni Miongoni Mwa Kundi ambalo lina fanya Njama Kwa Kufanya Vitendo Vya Kigaidi ambavyo ni
Kushiriki katika Kulipua Vituo Vya kuuzia Mafuta
Kukata Miti na Kuweka Barabarani, Kulipua maeneo yenye Mkusanyiko wa watu na Kuhamasisha Maaandamano ya siyo na Kikomo.
Mtobesya: Ni hizo Taarifa tu au Mlikuwa na Zingine?
Shahidi: Kimyaaa
Mtobesya: Ni nani aliwasaidia Kuwapa Taarifa Mpaka Mkajua Eneo alilokuwa Ling'wenya?
Shahidi: Nilikuwa na Mkuu wangu Afande Kingai yeye Ndiye alikuwa anajua aliyekuwa nampa taarifa
Mtobesya: Nitakuwa sahihi Kwamba Mpelelezi yoyote kabla hajafanya Upelelezi anakuwa na dhana Kichwani unapoenda Field Unaenda kuthibitisha Kama ni Chanya au Hasi ni sahihi?
Shahidi: Ni sahihi
Mtobesya: Mueleze Mheshimiwa Jaji Kwenye Shauri hili Dhana yako ilikuwa ni nini
Shahidi: nilikuwa naenda Field Kuthibitisha tuhuma kama Mtuhumiwa huyo anahusika
Mtobesya: Mueleze Mheshimiwa Jaji ilichukua muda gani, tangu unatengeneza Dhana hiyo Mpaka Mnamkamata Ling'wenya
Kimyaaaaaaaaaa kinatawala kwa sekunde kadhaa hapa... Namna gani!
Jaji: anamuuliza Shahidi kama ameelewa Swali
Shahidi anapata kigugumizi kidogo anashindwa kuongea hapa..
Lakini anafanikiwa kuendelea..
Shahidi: Ni palepale nilipopata Taarifa na Kuanza Kutafakari na haikuchukua Muda Mrefu
Mtobesya: Mueleze Jaji Taarifa hizo ulizipata lini
Shahidi: Siku ya Tarehe 04 August 2020
MTOBESYA: na Ling'wenya Mlimkamata tarehe ngapi?
Shahidi: Naomba nirejee Nyuma ya Swali Lako ulilokuwa Umeniuliza
MTOBESYA: enheeeeeeee!
Shahidi: UMENIULIZA Iinachukua Muda gani Kuniwezesha Kwenda Field
Mtobesya: Sijakuuliza Swali hilo
Shahidi: Dhana ni Kama Kitu ambacho huna a Uhakika nacho
Mtobesya: Hapana namaanisha HYPOTHESIS, Mpelelezi Yoyote lazima awe na Hypothesis
Shahidi: Kimyaaaaaaaaaa
Mtobesya: Nakurudisha Kwenye Swali Sasa, Je Mlimkamata lini Ling'wenya
Shahidi: Tarehe 05 August 2020
Mtobesya: Maelezo Ya Ling'wenya uliyaandika lini
Shahidi: Tarehe 07 August 2020
Mtobesya: Kwa hiyo nitakuwa Sasa Kwamba Wakati Unamuhoji ulikuwa na Taarifa
Shahidi: Hapana Sikuwa na Taarifa
Mtobesya: Siwezi Kukunyonga kwa Majibu yako. Haya Umesema Ling'wenya alikiri Kujihusisha Kufanya Vitendo hivyo ni Vipi
Shahidi: Kwamba kweli alijihusisha na Vitendo Vya kupanga Njama
Mtobesya: Nitakuwa sahihi nikisema Mpelelezi asiandike Maelezo ya Mtuhumiwa, Kwa sababu Mpelelezi anataarifa Nyingi Wakati anampeleleza?
Shahidi Hapana Siyo Sahihi
Mtobesya: Kwa hiyo pale ambapo Kuna Askari Mwingine na Mpelelezi Yupo Hairuhusiwi Askari Mwingine Kuchukua Maelezo
Kwamba Hamkuwezesha Kukutana na Ndugu..
Shahidi: Sahihi Sikusema
Mtobesya: Kwa hiyo tunakubaliana kwamba Nitakuwa sahihi nikisema Kwamba Mtu pekee anayejua kama Mtuhumiwa alikamatwa ni Nyie Mlimkamata, Yeye aliyekamatwa na Mtu aliyekamatwa Wakiwa Pamoja
Shahidi: Ni sahihi
Mtobesya: Unaelea nini Kuhusu Maelezo ya Onyo
Shahid: Ni yale yanayo chukuliwa Kuhusu Mtuhumiwa anahusishwa na Kutenda aina fulani ya Kosa
Mtobesya: Ni hivyo tu?
Shahidi: INATOSHA
Mtobesya: Nitakuwa Sahihi nikisema Maelezo ya Onyo Yanatakiwa Kuonyesha Mtuhumiwa Kosa analo tuhumiwa nalo
Shahidi: Ni sahihi
Mtobesya: Nitakuwa Sahihi Kwamba Kosa Unalomuonya Nalo ni lazima liwe limetamwaka Kwenye Sheria
Shahidi: Ni sahihi
Mtobesya: Nitakuwa Sahihi Kwamba Maelezo ya Onyo Yanatakiwa kuwa Sheria na inatakiwa Kuonyesha Kifungu Unachomuonya nacho
Shahidi: Siyo Kweli, unaweza Kumwambia Kwa Maneno tu
Mtobesya: Kwa hiyo siyo Muhimu Kumtajia Kifungu unacho Muonya nacho?
Shahidi: Ni Muhimu kwa Minajiri ya Kumuonya mshtakiwa Mwenyewe
Mtobesya: Kwa hiyo kwako wewe Siyo Muhimu
Shahidi: Nilisahau lakini nilikuwa nishamwambia
Mtobesya: Nitakuwa sahihi Kwamba ni Matakwa ya Kisheria, Baada ya zoezi la Kuonya Kuisha Tarehe, Mwaka na Muda lazima viwe katika fomu unayotumia Kumuonya
Shahidi: Ni sahihi
Mtobesya: na wewe Uliweka hivyo
Shahidi: Ndiyo Niliweka
Mtobesya: Tutaona baadae kama Uliweka
Mtobesya: na nitakuwa Sahihi Muda wa Kuonya Siyo Muda wa Kuchukua Maelezo, Unamuonya kwanza kisha Unamchukua Maelezo
Shahidi: Ni sahihi
Mtobesya: Kwa hiyo ni sahihi Kwamba muda wa Kuonya ni Tofauti na muda wa Kuchukua Maelezo
Shahidi: Ni sahihi
Mtobesya Twende kwenye Hitimisho la Kuandika Maelezo pale unapotakiwa Kuthibitisha
Nitakuwa Sahihi nikisema Ufungaji wa Maelezo ya onyo una namna Mbili au Tatu kwanza wa Mtu anaye Jua Kusoma na Kuandika na ameridhia Kwa anaye andika, ambaye ajui Kusoma na Kuandika au amekataa na Mwisho Mtu ambaye amekataa
Shahidi: Siyo Sahihi
Mtobesya: Haya tueleze Wewe Wa kwanza anathibitisha vipi
Shahidi: Yeye Mwenyewe anaandika Kwamba nimeyasoma na Kuyaelewa
Mtobesya: na hiyo inaonekana katika Statement uliyoiandika
Shahidi: Kimyaaaaaaaaaa
Mtobesya Twende kwenye Hitimisho la Kuandika Maelezo pale unapotakiwa Kuthibitisha Nitakuwa Sahihi nikisema Ufungaji wa Maelezo ya onyo una namna Mbili au Tatu kwanza wa Mtu anaye Jua Kusoma na Kuandika na ameridhia Kwa anaye andika, ambaye ajui Kusoma na Kuandika au amekataa na Mwisho Mtu ambaye amekataa Shahidi: Siyo Sahihi Mtobesya: Haya tueleze Wewe Wa kwanza anathibitisha vipi Shahidi: Yeye Mwenyewe anaandika Kwamba nimeyasoma na Kuyaelewa Mtobesya: na hiyo inaonekana katika Statement uliyoiandika Shahidi: Kimyaaaaaaaaaa
Mtobesya: na wewe Mwenyewe Unaandika Je Mwishoni
Shahidi: Unathibitisha Kuandika Maelezo ya Mtuhumiwa huyo
Mtobesya: huyo ambaye amesoma na kuandika, anathibitisha Vipi..? KWA signature na Dole Gumba Maana havitumiki kwa Pamoja
Shahidi: Alisaini Pamoja na Dole Gumba
Mtobesya: Kule Chini Mnapoweka Ithibati Kuna Vifungu Mnaviandika
Shahidi: sahihi
Mtobesya: Mueleze Jaji kwenye Maelezo yenu Mlitumia Vifungu gani
Shahidi: Ilikuwa Imeshaandikwa Kwenye Karatasi, niliona hakuna haja ya Kuweka hiko Kifungu
Mtobesya: Kitaje Kifungu
Shahidi: Kilikuwa Kifungu Cha 57(3)
Mtobesya: Umekitaja Maana Yake unakifahamu Mueleze Mheshimiwa Jaji kama hicho Kifungu aya zake
Shahidi: Sikumbuki Kama Zipo hizo aya
Mtobesya: Mheshimiwa Jaji naomba nipatiwe ID 1
Mahakama inampatia Mtobesya ID1
Mtobesya: Na Kuonyesha Kielelezo Cha Mahakama Nikuulize Maswali Machache, Iambie Mahakama Kama Baada Onyo Uliweka Muda
Shahidi anakuwa mbishiiiii hapa, Mbishi, lakini Mwishoni anasema HAKUNA MUDA..
Mtobesya: tuonyeshe uthibitisho amesoma na Kuyaelewa Sehemu gani
Shahidi: Mtuhumiwa amesaini na Kuweka Dole Gumba
Mtobesya: na Kifungu cha Sheria
Shahidi: Ndiyo nimesema Kwamba Karatasi ilikuwa Tight sikupata nafasi ya kuweka
Mtobesya: Mueleze Mheshimiwa Jaji Pale ambapo Maelezo ya Mtuhumiwa anathibitisha Kuna Kifungu cha Sheria au Hakipo
Shahidi: Hakipo Kifungu cha Sheria