Eehehehe wacha ncheke kwanza.....
Patq picha wanandoa wote ni waumini wa dini moja na wanashiriki vizuri ibadani.
Ghafla mmoja wa wanandoa anapitia changamoto kazini na anafukuzwa kazi. Anajaribu kutafuta kazi nyingine hapati, kila akijiajiri hola anaambulia hasara.
Anakutana na rafiki anamwambia ampeleke kwa fundi(mganga) sio bure amechezewa...
Wanapanga mipqngo yote ana anaweka imani atafanikiwa akitoka huko.
Wanandoa hawa hawajawahi kushiriki wala kiwa na imani na waganga wala ushirikina. Anarudi anamwambia mwenza wake kuhusu kwendq kwa mganga, mwenza wake hakubaliani na hilo wanakosana na anamwambia nenda ila mimi sijaafiki na usinihusishe na hiyo ibada sitaki kushiriki.
Jamaa anaenda kwa mganga anarudi na marundo ya dawa za kienyeji, sijui ya kunywa, ya kuoga, ya kupaka, yakutafuna basi tafrani. Mwenzake anamwambia tenga vyombo utavyotumia na madawa yako sitaki watoto washiriki kwa namna yeyote ile.
Jamaa anakuwa kiburi anataka mke amchemshie dawa zake eehehehe mke anamwambia sishiriki ibada za sanamu nilishakwambia ukitaka mwambie dada akutengenezee... mzozo ila mwanaume anakaza kichwa anaendelea na dawa zake.
Eehehehee usiku mwanaume anataka unyumba, mwanamke anamwambia umetoka kufanyiwa madawa na mengine unaendelea kunywa na kujipaka tafadhali maliza madawa yako ndo tuendelee sitaki kujihusisha na hizo ibada, nikishiriki tendo na wewe nakuwa nimeunga nafis yako na yangu kwenye hizo ibada tafadhali naomba umalize matibabu yako utanikuta nakusubiri.
Mwanaume anasema siwezi kusubiri wiki mbili, maana dawa anatumia kwa wiki mbili. Hapo unafikiri kunyima unyumba ni kosa ama ndo migogoro ya ndoa....
Bado hujakutana na mwanaume ametoka kunywa wanzuki yuko tip amelewa na amejikojolea anafanikiwa kurudi nyumbani anadai unyumba, tena kwa kelele... weee mama sikununu, panda juu uchezee koki hiyoo..... huku anapiga kwikwi.... mwanamke anatoa msonyoo wa kinaijeria halafu anajifunika tenge lake analala...
Je hii nayo ni migogoro ya ndoa?
Au ndo ile inasemwa kwa shida na raha?
#kataa ndoa mpoo...!!??
All in all, hakuna mwanadamu aliyekamilika ikiwemo mimi na wewe. Wote tunachukuluana na wengine wanashida ya akili ila sababu wanapata nyege huwezi kiwazuia kupata wenza, itakuwa ni ukatili wa hisia.
Alnuru,
Kasinde Mahaba 😉.