Kesi ya Agnes Doris Liundi - Nini hasa kilitokea?

Hili tukio liwe ni fundisho kwa wanandoa wote. Ndoa ni taasisi na iheshimiwe na watu wote. Msingi mkuu wa ndoa ni UPENDO,ukimpenda mwenzio hautomuwazia au kumtendea mabaya.
 
Dah, ningekuwa judge hakika ningemuonea huyu mama huruma.
 
Bonge la precedent kwenye criminal law kuhusu ishu za insanity, thnx
 
ALIYEKUWA Msajili wa kwanza wa vyama vya siasa, Jaji George Liundi, amefariki dunia juzi mchana nyumbani kwake Keko Juu jijini Dar es Salaam. Akizungumza na Tanzania Daima, mtoto wa marehemu, Taji Liundi, alisema baba yake alifariki dunia saa 7 mchana baada ya kuugua malaria, shinikizo la damu na maumivu ya mgongo.

Taji alisema taratibu za mazishi zinafanywa na familia nyumbani kwao Keko Juu, ambapo marehemu Liundi anatarajiwa kuzikwa Alhamisi katika makaburi ya Chang'ombe. Enzi za uhai wake marehemu Liundi alikuwa msajili wa kwanza wa vyama vya siasa, ameacha watoto watatu na wajukuu wanne.

Akiwa Jaji, Liundi alipitia hatua ngumu kwenye maisha yake, baada ya mkewe Agnes Doris Liundi kushitakiwa na Jamhuri mwaka 1979 kwa kosa la kuwaua watoto wake watatu kwa kuwanywesha sumu Februari 21,1978 nyumbani kwao jijini Dar es Salaam.

Katika kesi hiyo iliyokuwa mbele ya Jaji Lewis Makame, Agness aliyeolewa na Liundi mwaka 1967 alihukumiwa kunyongwa hadi kufa.

Source:
Tanzania Daima – Jaji Liundi afariki dunia

CC: Mtambuzi,
[MENTION]JokaKuu[/MENTION], [MENTION]Joka Kuu[/MENTION], [MENTION]RR[/MENTION], NATA, ram, Asprin, Mwita Maranya, Pasco, Mentor, Mama Joe, magee, FirstLady1, The Boss, [MENTION]JS[/MENTION], Kidogo chetu, Lukolo, Bigbro, Mtumishi Wetu, Leftist, B'REAL, Kombo, kadoda11, kanga, GIUSEPE, BPM, MAHEPE, Kongosho, mkomatembo, ALEX PETER, webondo, Ronn M, Kijivo, sober saimoni
 
Last edited by a moderator:
Dah, ningekuwa judge hakika ningemuonea huyu mama huruma.

Ndiyo maana siyo judge! Sheria haina huruma ndugu, na judge siye anayetia mtu hatiani, sheria ndiyo inamtia mtu hatiani! HUYO DADA ALIONESHA UKATILI WA HALI YA JUU NA ALISTAHILI KUNYONGWA!
 
Mkuu Mtambuzi nimesahau kuuliza, kwa hiyo hiyo hukumu ilishatekelezwa? Au mama bado yuko jela, au alifariki natural death? Na kama alifariki natural death alifia jela au wapi? Samahani, ni OP kidogo.
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…