Kesi ya akina Mbowe ina manufaa gani kwetu CCM, mbona haitupi any political mileage?

kaka, hii kesi ina manufaa kwa CCM mwendazake - tatizo maza anataka kurithi kila kitu hadi matatizo binafsi ya marehemu kitu ambacho ni kosa kubwa kibinadamu hata katika ulimwengu wa kiroho.

Maza apewa ushauri huu muhimu, kama marehemu alikuwa hampendi A, B, C D basi ni yeye na wala asitake sisi wana CCM wote tuendelee kuyaachukia ambayo yeye aliyona hayamfani wakati yeye hayupo duniani na hawezi kurudi tena.

Hata kama marehemu aliapa kutotoa katiba mpya basi ni yeye, sasa kwani sisi tulibaki hapa duniani tukisema katiba mpya ni ajenda yetu leo ni kosa ? arudi basi kama ana uwezo huo.

Narudia tena, maza ashauriwe - adui wa mtangulizi wako si wa kwako, principal ya maisha ni kwamba tengeneza marafikio wengi kuliko maadui.

Nitamweshimu wana CCM YEYOTE atayetamka kwamba katiba mpya ni ajenda yetu ya leo, regardless !!
 
Wengi wanajua km Mbowe anafadhaika SANA kuwa gerezani, lkn ukweli ni kwamba Mbowe anafurahia sana kuwa gerezani kuliko kuwa mtaani aki organize masuala ya katiba mpya.

Mbowe hapo anafanya siasa ki sayansi sana kwa gharama kubwa ya CCM
Mbowe ni janja sana kuplay victim of current political climate ukijumlisha na shuhuda za mashahidi na watuhumiwa ndio kabisa wanaivua nguo system ie CCM/Serikali
 
Kama kuna watu hawana akili nchi hii ni Usalama wa Taifa waliopandikizwa ndani ya CCM. Hawa ndio Mainjinia wa hii kesi uchwara. Mnawaona kina Kingai na Jumanne ni Punda tu wabeba mizigo na kama mnavyowaona wamelemewa na Sasa la lawama zote ziko juu Yao kumbe waanzilishi wa Msala wako pembeni.
 
Nakubali
 
Umeongea vizuri nimekuunga mkono sana
 
Sabaya yu gerezani.
Alitaka kumuua mbowe akasahau magufuli ni binadamu.
Asante mungu kwa maajabu aliyotenda 17.3.2021
 
Imesaidia yafuatayo

i)Hakuna Uhuru wa mahakama Tanzakiza

ii)sheria kuvunjwa waziwazi(Police,mawakili wa serikali & jaji)

iii)Uzwazwa wa majaji na mawakili wa serikali licha ya kujifanya wasomi na watu wenye weledi

iv)Ukatili wa police-CCM na Uongo wao

v) JWTZ nako hakuna haki

Mengine GT wataongeza
 
CCM inahusika vipi na hii kesi ya Mbowe?
CCM inahusiana na Mbowe kwenye Ubunge- walimtoa akiwepo jimboni hai
CCM inahusiana na Mbowe kwenye Urais- walimshinda akiwa hayuko jela
CCM haihitaji Mbowe afungwe ndiyo ipate inachokitaka kwa sababu imekuwa ikipata akiwepo
 
Hii kesi imesaidia katika vita vya kiuchumi dhidi ya mabeberu wa bunge la ulaya.Tutapigana nao
 
Hii kesi imekuja na faida nyingi kwa watanzania hasa wapenda haki. Imesaidia wasiojulikana wako wazi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…