Kesi ya Babu Seya na wanae - Ukweli ni upi haswa?

jamani namuonea babu seya na mwanaye huruma but kama ni kweli walibaka Mungu asiwakumbuke but kama wanaonewa Mungu aliye hai na awatazame kwa jicho lake la huruma
 

kitumbo kumwombea mkosefu msamaha hakutaondoa wala kuathiri uadilifu wangu! Kama Jamhuri haijawai kunituhumu wala kunishitaki kwa kosa lolote basi bado mi ni mwadilifug,pia mwadilifu mbele za Mungu wangu. Kitumbo ukisoma mada jitaidi kuelewa wala si kumeza,angali mfano ulivotumika wala si kukurupuka. Pia mfano wangu haujataja Barnaba,nimesema Barabba,au leo umejiandaa kutonielewa? Nielewe mkuu,hata wakosaji wanaitaji msamaha na upendo wa kweli!
 

Hivi ingekuwa ni mwanao wa miaka 10 amefanyiwa mambo machafu (Amelawitiwa) na huyo Nguza bado ungeandika upuuzi kama huu?.
 
Kama babu seya alipatikana na atia, basi watu kama yeye si wakusamehewa kamwe na iwefundisho kwa wanaume wote wenye tabia kama ya babu seya!
Tabia yao ni mbaya na yakiuaji!
 
Gsana unajua Mh JK huwa anatoa msamaha kwa wafungwa wa aina gani?how far are u sure kama hana hatia,wabongo bwana kwa kupenda kusikiliza maneno ya vijiweni!
 

Vigezo vya msamaha - wasiwe wafungwa wa makosa ya kutumia silaha, ubakaji....
 
Jamani msisikie, kupigiwa kunauma,hata ingekuwa mimi ningemrostisha babu Seya, yaani mahali mkuu anapumzikia yeye akafanye pumziko lake, hapana wacha aozee huko hyko lupango.
 
Gsana...

TUko pamoja sana, ila naomba unielewe kwamba iwapo mkosaji ameiba kuku au kajeruhi kwa momentary insanity naweza kuelewa... lakini kama mtu amelawiti watoto zaidi ya kumi na kuwaharibu for the restof their lives, huyo kwangu ningenyonga, unasema hivyo labda huna watoto... hapa simzungumzii nguza kama nguza nazungumzia mtu atakayekuja na kuanza kulawiti wanangu tena under 10 years of age

na ndio maana nikasema apewe haki yake; binafsi ni mshabiki wa nyimbo zake sana tu na kwa maestro kiki hunikosi hata anapopiga kigamboni jumamosi mchana

JE UNA WA WATOTO, UMESHAWAHI KUPATA TASWIRA MWANAO MDOGO, MALAIKA AS HE/SHE CAN BE ANARUDI NYUMBANI AKIWA KAHARIBIKA KABISA HUKO NYUMA?

LA NGUZA LINA SIASA NA VISASI NDANI YAKE KWAHIYO WAWEZA USIWE MFANO MZURI
 
Vigezo vya msamaha - wasiwe wafungwa wa makosa ya kutumia silaha, ubakaji....
mKUU THANKS

NAPATA SHIDA SANA KUMWELEWA GSANA

Hivi kweli mtu amebaka watoto wako au mkeo, unaweza ukasema awe huru? [ANAGALIZO, HAPA NAZUNGUMZIA GENERAL SITUATION NA SI YA BABU SEYA]
 

Mkuu Heshima kwako,
Binafsi sijawahi kusikia Babu Seya kakiri kosa lake, ninachojua mimi kuna utata mwingi sana juu ya shauri lilomtia hatiani pamoja na familia yake, siwezi kusema ni nini maana sielewi na ninapo fikiri juu yake huwa nachanganyikiwa.

Waliomtia hatiani wanajua ukweli wake, hivyo wamtendee haki kwani pia anastahili.
 
This time anatoka Liyumba....maana ametumikia kama mwaka nusu hivi akiwa mahabusu...na amefungwa miaka 2....lazima atoke dec....hii..atakuwa uraiani soon ila najuaa ata seek ile hukumu yake isomwe tu akishinda...ajisafishe kama Rage......maana huwezi juaa labda baadaeataenda kwenye siasa......
 
mKUU THANKS

NAPATA SHIDA SANA KUMWELEWA GSANA

Hivi kweli mtu amebaka watoto wako au mkeo, unaweza ukasema awe huru? [ANAGALIZO, HAPA NAZUNGUMZIA GENERAL SITUATION NA SI YA BABU SEYA]

Wafungwa wanapata mshamaha wa raisi kwa vigezo mfano wenye vifungo vya muda mfupi, wagonjwa ,,,,,,,,mwisho huelezwa kinagaubwaga kuwa wafungwa wa makosa x,y,z msamaha hauwahusu. Mr President hawezi fanya "Isolation" wala hatoi msamaha kwa kuangalia mtu bali ni kwa wale wanaofikia vigezo vilivyowekwa
 
Gsana unajua Mh JK huwa anatoa msamaha kwa wafungwa wa aina gani?how far are u sure kama hana hatia,wabongo bwana kwa kupenda kusikiliza maneno ya vijiweni!
maneno ya vijiweni?how far are u sure kama hana hatia?...ivi umesoma nilichoandika mkuu? Kuna sehemu nmesema hana hatia au ana atia,mi si court! Ivi mkuu huwa unakaa na kupitia mambo muhimu kama "powers of the president?", kumbuka kupitia sheria kidogo,si kudhania! Remember no law without except! Rais anaweza kuondoa au kubadilisha au kupunguza au kubatilisha kifungo chochote! Soma hata katiba inaeleza vizuri wala usipate ugumu wa kunielewa,ila aya ni maoni yangu,kama si mazuri yapuuze tu.
 

mkuu pata nakala ya court rule ya kesi ile utapata moral decision bila kusumbua ubongo,holding other factors equal nadhani ni fair usemavo,ila ukichunguza mazingira yote,ubakaji huo haupo. Alaf mkuu nakuacha na swali,ktk sheria za ubakaji Tanzania,unaweza kupata japo kifungu kimoja kinachowakuta hatiani kama "group rape?" . Mwanaume m1 anaweza kubaka m/mke 1 na/au wengi ila si wanaume wengi kumbaka m2 mmoja! Wa kwanza kubaka ndo anakumbana na sheria! Mbona wa2 wanakuwa wagumu kujua sheria? Usipate tabu kunieleza yani tukienda kisheria mbona patachimbika? Ila mambo mengne tunafunika tu! Mwisho,naheshimu mawazo ya wengi kama wataona Babu asirudi huku uraiani,ni sawa tu.
 
waachiliwe waovu wote/kwani kuna wakati mh....alisema hao wanafunzi wanaopewa mimba ni VIHEREHERRE VYAO VIMEWAPONZA HAhaaaahaaaa yupo makini sana anatufaa sana
 

naungana nawe,ili kuna sehemu baada ya appeal kufail pale alipoachiwa mmojawapo waliobaki waliomba msamaha kwa kuandika barua kwa rais. Ukiomba msamaha,kwanza unatii ndo msamaha unaombwa,ukitii unakubaliana na makosa. Ndo maana nkasema walikubali makosa. Tupo pamoja mkuu!
 


Gsana, kwanza utueleze uhusiano wako na babu seya family ukojee vinginevyo ningekuelewa kama ungewatetea 'wabakaji' wote walioko lupango, ingawa ni kweli kwa washabiki wa babu seya inauma sana
 
Hakika yeye mwenye mamlaka ya kusamehe ataamua na hakuna atakayepinga. Naogopa kutenda makosa duniani, maana nitaadhibiwa duniani na huko mbinguni itakuwa mara mia elfu na elfu.
 
Hakika yeye mwenye mamlaka ya kusamehe ataamua na hakuna atakayepinga. Naogopa kutenda makosa duniani, maana nitaadhibiwa duniani na huko mbinguni itakuwa mara mia elfu na elfu.

Ina maana miaka yako yote ulioishi hujawahi kutenda makosa yoyote?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…