Kesi ya Babu Seya na wanae - Ukweli ni upi haswa?

Mtoa mada usilinganishe kesi ya babu Seya na mtu alieenda Kisongo baada ya kuvuta bhangi
 
Interestingly bado kuna watu wanaamini kuwa Babu Seya alionewa. Ama kweli imani ni kitu kingine! Lakini tunachojua wengi wetu ni kuwa vyombo vyote na mfumo mzima wa kutoa haki ulithibitisha makosa yake, na kumwadhibu ipasavyo. Rufaa zote hali kadhalika. Rafiki zangu wataalamu wa maradhi ya akili waliniambia kuamini kitu kinachopingana kabisa na ukweli wote na ushahidi wote uliopo ni ugonjwa, wenyewe wanaita 'delusion'. Labda kuna 'mass delusion' inayohitaji tiba hapa.
 
Funzo kutokana na suala hili
Mosi.usipende kula vya mwenzako na hasa ukikanywa.kwa kuwa hutajua ataamua kukupa adhabu gani na kinyngo kitakwisha lini
Pili.maamuzi ya hisia si mazuri.
Tatu.ukienda kwa watu fuata masharti ya watu ukiona hwezi rudi mapema kwenu pasipo kuvunjiana heshima.

Nne.ukweli hauna mbadala...mshahara wa dhambi ni mauti
 
Nakusihi ili ujue ukweli wa yaliotokea hadi hao wapendwa wetu wakashindwa rufaa zao zote kafanye utafiti wale watoto wapo, wazazi wao wapo na hata waalimu wa mugabe primary school bado wapo wasiliana nao ili ujiridhishe na ukweli wa yaliotokea!mimi kwangu namchukulia msamaha walio uomba mbele ya aliyekuwa waziri wa mambo ya ndani Mh Chikawe kwamba akawaombee kwa raisi kwamba kwa miaka waliyokaa ndani wameshajifunza vya kutosha! Kwa hiyo wameomba raisi awape msamaha na hawatarudia tena!mwisho wakunukuu
 
Unaongeza tu contradictions. Shule iliyotajwa kwenye kesi sio Mugabe bali Mashujaa...
 
Daah hata Mimi hii nashindwaga kuielewa kabisa eti baba na wanae wana to mi shundundu wakika fanyia katoto kadogo kwakupokezana mmh?
sijui labda ushirikina yaan nahisi hata shetani angegoma huu ufirauni baba na watoto kwa vitoto vidogo
 
Haki duniani...nikama ngamia kuingia tundu la sindano..60% za kesi wengi kwa kusngzwa
 
Mimi binafsi nilikua bado mdogo katika kipindi cha mashtaka dhidi ya Babu Seya na mwanae.Lakini kutokana na stori tofauti kitaa.....Nimeona niulize nn ukweli??
 
ANGALIZO : katika hali aliyo nayo Nguza Viking anaweza kumuita rais jina lolote...anaweza hata kumuita ni mwakilishi wa mungu hapa duniani.so tusimhukumu kutokana na maneno aliyotumia au rais aliyemwandikia. jukwaa hili ni la Intelejensia tuangalie mambo haya ki intelejensia zaidi tuweke emotions zetu pembeni.


Miaka hiyo kesi hii imetokea asilimia kubwa ya wanajamii forum walikuwa wadogo au watoto. lakini ni moja ya kesi ambazo zilikuwa gumzo kutokana na mhusika mwenyewe kuwa alikuwa akifahamika na pia suala la kuhusishwa yeye na familia yake nzima na kitendo cha ubakaji watoto.

ni mengi ambayo yalikuwa yakisemwa kuhusiana na mwanamuzi huku Nguza Viking au maarufu kwa jina la Babu Seya na watoto wake watatu. iliwasha maskioni mwa watu, watu walizungumza kila walilozungumza. kwa wazazi waliokuwa na watoto waliumizwa sana na kesi hii wakichukizwa na kitendo cha kikatili ambacho ilisemekana kilifanywa na Familia hii ya Nguza Viking.

inasemekana kuwa yeye na familia yake walikuwa wakiwabaka/lawiti watoto wadogo. hapa kulikuwa na maswali mengi sana kwa mzazi kufanya kitendo hiki akishikirikiana na watoto wake watatu.ilileta ukakasi sana. na hivyo akajikuta yeye na watoto wake watatu wakihukumiwa kifungo cha maisha.

ukiwaza unaweza sema kama walikuwa wakifanya kitendo hicho basi walifanya hivyo wakiwa chini ya influence ya kitu flan..landa ni ulevi au iman za kishirikina. sababu katika hali ya kawaida ni ngumu sana. lakini yalitokea hayo mambo hayo kwa mujibu wa mahakama. miaka mingi imepita Nguza Viking alionekana ni mtu ambaye hakuridhika na kesi au hukumu ile. na mara nyingi amekuw aakijaribu kukata rufaa na mwishowe angalau alipata faraja ya watoto wake wawili kuachiwa baada ya kuonekana hawakuwa na hatia. ila yeye na mwanawe mmoja walirudishwa tena ndani.

bado mpaka leo hii Nguza Viking anaonekana ni mtu ambaye hakuwah kukubaliana na ile hukumu au kesi. na kumekuwa na mingo'ono mingi sana kuhusiana na ile kesi.wengine wakisema kuwa ilikuwa ni adhabu baada ya kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mwanamke mmoja aliyekuwa akitembea na kigogo mmoja.ikaonekana apewe adhabu hiyo.

suala hili kwa kifupi lilizungumzwa kwenye uchaguzi wa mwaka 2015 mgombea mmoja alidokeza tu kifupi kuwa angemtoa babu seya gerezani. watu wengi hawakuataka kufuatilia kwa nini aseme vile mtu ambaye alikuwa huko nyuma kwenye serikali? je alikuwa na siri gani kuhusiana na kufungwa kwa familia hii ambayo hakuweka wazi?

ni kwanini waandishi hawakutaka kumuuliza kwa nini amtoe babu seya wakati mahakama ilikuwa imemhukumu kuwa ni mkosa?watu hawakutaka kuangalia zaidi.hawakutaka kwenda mbali zaidi waliishii sana sana kukebehi na kusahau kuwa huyu mtu ikiwa kweli alikuwa hana makosa alistahili kupewa haki ya kuishi huru.

katika nchi zeu za kiafrika (sijasema tanzania) wakati mwingine siasa zimekuwa zikitumika vibaya sana na nguvu za kisiasa zimekuwa zikitumika kwa maslah binafsi. lakini tumekuwa wasahaulifu sana. kawaida watuhumiwa wengi baada ya kuhukumiwa huwa wanajua maisha yao yameishia pale. lakini kwa nini mpaka leo nguza viking anaamini hajaetendewa haki na kuomba rais aingilie kati?ni kwanini?tumewah kujiuliza jambo hilo?au ni kwa kuwa sisi tupo huru hatujui waliofungwa wana hali gani?mimi sikatai kama ana makosa basi apate adhabu stahili. kuna wafungwa wangapi ndani ambao pamoja na kuwa walikana mashtaka lakini walipofungwa wakakubaliana na ukweli kuwa walikosea?

nimeiona barua inayosemekana kuwa imetoka kwa nguza viking. nimeisoma... concern yangu ni je ni kweli alikosa? je kama hakukosa ilikuaje? je kwa nini anadhani amejifunza kutokana na makosa? je kuna uwezekano kama kweli alikosea rais akamsamehe?au kama hakukosa kesi yake ikasikilizwa tena kwa kutumia mahakimu na mawakili wengine?

mimi sijui. bado kuna siri au ukweli flan ambao hatukuwah kuupata katika kesi hii. tusiangalie sana alichokiandika.katika hali aliyo nayo anaweza kumuita rais jina lolote..anaweza hata kumuita ni mwakilishi wa mungu hapa duniani.so tusimhukumu kutokana na maneno aliyotumia au rais aliyemwandikia. jukwa hili ni la Intelejensia tuangalie mambo haya ki intelejensia zaidi tuweke emotions zetu pembeni.
 
Kumbe Gududuu ukiweka bia na madem pembeni unakuaga GT..
Hongera sana mzee wa madem
 
Hapo umeongea kitu kikaniingia akilini.sijui nitawasaidiaje jamaa hawa.
 

binafsi kufungwa na hukumu hii hainiingii akilini hata kidogo. kuna muda unajaribu kuangalia kwa jicho la kibinadamu na mambo yanakua mazito kama mguu wa tembo.
ila yuko Mungu na kwake kila zito kwetu hulitua. iko siku kama hawa jamaa hawakufanya hili suala basi mmoja wa walioko kwenye uo msuko wa kuwasukia kesi atajitokeza na kuyaweka yote bayana.
Mungu huwa hamtupi mja wake, hungojea muda muafaka wa kufanya maaamuzi.
 
Jamaa hawakujua aliye nyuma ya hiyo kesi, wakawa wanatamba the first day wanamatwa na kupelekwa osterbay police, unajua ukishakuwa maarufu. Kifupi ni kweli kwamba waliwafanyia wale watoto huo mchezo.

Sasa wale wengine inasemekana walikuwa under age wakati wanatenda na pia kuhukumiwa na ndio maana wakaachiwa.
 
baba angu alishiriki katika upelelezi wa hii kesi.anasema ktk interrogation na watuhumiwa walikiri kuhusika..anawashangaa watu wanavolichukulia hili swali kisiasa.
Mzee wako ni Police? Tafadhali mwambie RAIA wanahasira sana na wao ni vile tu wanakautamaduni kauoga!
 
Aiseeeeee...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…