Kesi ya Babu Seya na wanae - Ukweli ni upi haswa?

Wazee Hili suala si la kuingia kichwa kichwa.... Kama walifanya malipo yao ndio hayo na kama hawakufanya ukweli utathibitika hata kama Nguza na wanawe watakua wamekufa!!!
Mshahara wa "dhambi ni mauti"
 


Huyo mwanamke sidhani kama atajitokeza, hasa baada ya kusema kwamba ameokoka; ingawa inatia shaka kuona mlokole kashindwa kutubu kwa jamii kuhusu kupoteza watoto wa watu
 

Mkuu hapa JF watu iwa tunaongea kwa ushahidi na kumwaga evidence kama wewe upo karibu na hilo file kwa nn usiscan na kisha ukaliweka hapa kila mtu alisome kisha tujue ukweli ni upi na uongo ni upi.
 

Ukitaka kujua Mungu anaweza,look at Mahita now though it was planned look like a normally KUSTAHAFU lakini watu waliupata ukweli.

Na ile rumor ya kwamba amekua grounded nyumbani kwake nadhani uliisikia?

Kwake M/Mungu haya ni madogo nawafanyao maovu huwaumbua hapa hapa you will see na mtakua mashaihidi wa hili.

BUT,insist wakina Nguza wawe hawakufanya hichi kitendo zaid i yakusingiziwa which me too believed wamepakaziwa .

"You are liable to fallin the ditch you dig for others".....Rumi masnevi
 
Hapana ... hawakupakaziwa ... hawa watu walicheza mkanda wa mambo hayo na watoto .. mkanda ukauzwa nje ya nchi .. some foreign ambassodor to tanzania had gone back home on an errand ... akaufuma huu mkanda ambayo aliletewa akaambia see what is happening in Tanzania ... the ambassodor who knew the culprits came back to TZ ... called top officials and showed them the mkada ... luckily the guys were easily identified ... and the only thing to do was to pin them down ...wakatumia hizo mbinu as wale watoto waliyowachezea wasingepatikana .. this is why hii kesi no one could tamper with with it as there was recorded evidence ....

They are paying for their sins
 

mambo ya kutatanisha kwenye hili bado ni mengi na ukweli umefichwa mbali inavyo elekea.
 

Mhh!!!!!!!!!!!!!
 
Hapa umechanganya madawa mkuu, nenda ukaangalie tena vizuri ni kigogo gani hasa anayehusika.

Hata mimi najua ni kigogo mwingine, na bado yuko madarakani, tena madaraka makubwa ya nchi hii.

Hivi hawa wafungwa wa kuonewa sasa wako gereza gani? Mimi nilisikia waliachia wakarudishwa kwao Congo DRC!
 

Amini usiamini huo ushahidi ulichongwa na ukachongeka!
 
Mkuu vipi Mwalimu aliyekuwa akiwapeleka watoto hao kuachiwa bila hatia, mbona hiyo inakuingia akilini?

Halafu ninaomba ufuatilie tena kwa makini je hawa wakongo bado wapo jela kweli, au? Msiwe mnakurupuka wakuu!

Mimi nilisikia wako DRC wakakabidhiwa kwa J.Kabila na wakaonywa wasirudi tena TZ.
 

Hii issue nimewahi kuisikia kiihivyo sasa sijui nani mkweli hapo.
Kama ndo hivyo basi ilitungwa ile kesi.
 

FP, hivi wewe unaishi tanzania ya wapi?! Yaani mpaka sasa hujui kwamba ushahidi mwingi tz huwa ni wa ku-forge!

Kama kweli unakwenda kusoma faili lenye ushahidi na hukumu iliyoandaliwa na vigogo basi wewe ni wa kuhurumiwa.
 

Can u prove it?
 
Suala la familia ile kuhukumiwa ki-vile inatia uchungu. Siwezi kutetea maovu kama yametokea ila vile vile kama kuna mtu amemuonea mwingine inabidi na yeye anyoshewe kidole.

Kuhusu sakata la babu Seya na watoto niliwahi kusikia kuwa alikuwa na utaratibu wa kuwaimbia nyimbo wanapokuwa kwenye mapumziko mafupi (breakfast). Na hivyo watoto wengi walipenda kwenda pale kuimbiwa nyimbo. Wabaya kwa kulipata hilo walilitumia kama mtego wa kumnasa huyo ndugu.

Kama suala lilikuwa kugombania mwanamke, hapo hakuna mwenye haki kwa kuwa wote hawakuwa na haki. Hata huyo aliyekuwa mbabe kwa kumuweka mwingine kifungoni, tena familia nzima inabidi atubu kwa kuwa katika uharibifu aliopanda yamo matunda yake. Kama haelewi kuwa Mungu anawashughulikia watu wa namna hiyo basi asome kisa cha Daudi na Uria.

umbea mwingine niliowahi kuupata ni kwamba mwanamke aliyekuwa akigombewa keshakuwa marehemu. Je, kuna mwenye habari?
 
Now it clicks ... read my version .. this guy alikuwa waziri wa mambo ya nje ... he was the right person to deal with this ... the other ambassador alimkabidhi yeye tape ...very true

Nikweli alikuwa waziri wa mambo ya nje ya nyumba yake. Lakini walitunga kesi.

Nakuhakikishia hakuna aliyeiona hiyo tape. Hata FairPlayer anayedai amesoma file la kesi leo hii ukimwambia akuletee hiyo tape ataingia mtini cause it doesn't exist on the earth! The case was fabricated by the kigogo na marafiki zake walioko tz na nje.
 


Leta vithibitisho vya kuonewa kwao ili tulionge lee, vipi kama ni kweli hawa watu walukuwa wakiwafanyaia vitendo vibaya wale watoto, ulishajaribu kujiweka upande wa mzazi

nadhani ni bora tiongelee bei za vyakula zinazopanda kiolela hapa TZ kuliko kuongelea vitu visinyo na ushahidi
 
Kujua kabati liko wapi, sio kithibitisho kuwa wameabkwa, pengine walikwenda kucheza na wenzao, au mwalimu wao aliwapeleka pale kwa lengo jingine na si hilo la kubakwa. Vipimo vya Daktari je vinasemaje? Na kwa nini huyo mwalimu hakufungwa?

kweli kabisa anaetaka lake inawezekana kuna mtu ambae anaijua vizuri nyumba yao na akafanya kazi ya kuwafundisha watoti semeni kabati lipo upande gani na huenda pia ni yule dada akiwa ameshikiwa mtutu na vitisho vingi akasema kila kitu hata kusema kama babu seya ana kovu sehemu fulani hivyo wakatumia kumaliza yeye na familia yake. kuna watu wanaishi kama miungu humu dunian huko kwa Mungu kesho sijui watafanyajwe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…