Kesi ya Boni Yai, Malisa yapigwa kalenda, kusikilizwa Desemba 19

Kesi ya Boni Yai, Malisa yapigwa kalenda, kusikilizwa Desemba 19

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
896
Reaction score
1,427
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imepanga Desemba 19, 2024 kuanza kusikiliza ushahidi katika kesi ya kuchapisha taarifa za uongo kwa lengo la kupotosha umma, inayomkabili meya wa zamani wa Manispaa ya Ubungo, Boniface Jacob (42) maarufu Boni Yai.

Mbali na Jacob, mshtakiwa wa pili katika kesi hiyo ya jinai namba 11805/2024 ni Godlisten Malisa (38) ambaye ni Ofisa Afya na mkazi wa Moshi Mkoani Kilimanjaro.

Jacob ambaye ni mkazi wa Mbezi Msakuzi na mwenzake Malisa wanakabiliwa na mashtaka matatu, ambapo mashtaka mawili kati ya hayo yamkabili Jacob peke yake.

Soma pia: Boniface Jacob, Malisa watua Kisutu kufuatilia kesi inayowakabili, yapangwa Agosti 29, 2024

Wakili wa Serikali, Asiat Mzamiru ameieleza Mahakama hiyo, kuwa shauri hili liliitwa mahakamani hapo kwa ajili ya kuanza kusikilizwa lakini hakimu anayesikiliza shauri hilo yupo likizo, hivyo anaomba tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa.

Hakimu Mkazi Mwandamizi, Godgrey Mhini aliahirisha shauri hilo akisema kwa kuwa hakimu anayesikiliza shauri hilo, yupo likizo, kesi hiyo anaiahirisha hadi Desemba 19, 2024 kwa ajili ya kuanza kusikilizwa.

Chanzo: Mwananchi
 
Back
Top Bottom