Kesi ya Diwani wa CCM Handeni yapigwa kalenda

Kesi ya Diwani wa CCM Handeni yapigwa kalenda

Suley2019

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Posts
2,203
Reaction score
5,610
Kesi ya Diwani wa Chanika wilayani Handeni, Tanga, Abdallah Chihumpu imeshindwa kuendelea baada ya hakimu anayeisikiliza kutokuwepo mahakamani.

Diwani huyo anashitakiwa kwa kosa la kumdhalilisha mfanyabiashara, Stanley Lyakundi kuwa ameiba eneo la wazi la Shule ya Msingi Chanika.

Shauri hilo kwa mara ya kwanza lilitajwa Machi 20, 2024 katika Mahakama ya Wilaya Handeni, leo Jumatatu Aprili 22, 2024, akizungumza mbele ya Hakimu mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Handeni, Veronica Siao, mwanasheria upande wa mlalamikaji, Tumwesigwe Kato ameiomba Mahakama iahirishe kesi hiyo baada ya hakimu anayetakiwa kuisikiliza kutokuwepo mahakamani hapo leo.

“Mheshimiwa Hakimu tunaomba tarehe ya mbele kwa sababu mheshimiwa anayetakiwa kusikiliza shauri hili hayupo leo,” amesema mwanasheria huyo.

Mwanasheria wa upande wa mlalamikiwa, Baraka Lusewa amekubaliana na maombi hayo na Hakimu ameiahirisha hadi Mei 17, 2024 itakapotajwa tena.
 
Back
Top Bottom