Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Kesi ya kusambaza taarifa za uongo kwenye Mtandao wa X inayomkabili wanasiasa mkongwe nchini, Dkt. Willibrod Slaa (76) itatajwa leo Februari 6, 2025 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam.
Dk Slaa anadaiwa kutenda kosa hilo chini ya kifungu cha 16 cha Sheria ya Makosa ya Mtandao namba 14 ya mwaka 2015.
Kesi hiyo inasikilizwa na Hakimu Mkazi Mkuu, Beda Nyaki na imeitwa leo Alhamisi, Februari 6, 2025 kwa ajili ya kutajwa na kuangalia iwapo upelelezi wake umekamilika.
Updates...
Kesi Namba 993/2025 inayomkabili Mwanasiasa mkongwe, Dkt. Willbroad Slaa (76), inayosikilizwa na Hakimu Mkazi Mkuu, Beda Nyaki, imeahirishwa mpaka Februari 18, 2025 ambapo iliitwa kwa ajili ya kutajwa na kuangalia iwapo upelelezi umekamilika.
Dkt. Slaa anakabiliwa na tuhuma za kusambaza taarifa za uongo kwenye Mtandao wa X ambapo inadaiwa ametenda kosa hilo chini ya kifungu cha 16 cha Sheria ya Makosa ya Mtandao namba 14 ya Mwaka 2015.
Ikumbukwe, Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini (DPP) amekata rufaa katika Mahakama ya Rufani, kupinga uamuzi wa Mahakama Kuu ulioelekeza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kushughulikia suala la dhamana ya Dkt. Slaa na kuangalia uhalali wa kesi ya jinai inayomkabili kwa haraka.
Soma, Pia: Dkt. Slaa ashindwa kufikishwa Mahakamani kutokana na changamoto za usafiri