Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Wakili Peter Madeleka anayemwakilisha Dk. Wilbord Slaa kwenye kesi Na.993 ya mwaka 2025 ya kuchapisha taarifa za uongo kwenye mtandao wa X ameiomba mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuuwajibisha upande wa Jamhuri kwa kutomfikisha mahakamani hapo mtuhumiwa (Dk. Slaa).
Madeleka amedai mahakamani hapo kuwa upande wa Jamhuri ndio uliowasilisha zuio la dhamana ya Dk. Slaa kwa madai ya usalama wake "ikiwa haonekani upo wapi uhakika wa usalama wake"
=====
Soma: Kesi ya Dr. Slaa inaendelea Mahakamani bila yeye kuwepo
Dk Slaa alisomewa kesi ya jinai namba 993 ya mwaka 2025 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Beda Nyaki.
- Dkt. Slaa afikishwa mahakamani Kisutu kwa Shtaka la kusambaza taarifa za Uongo