Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Kesi ya kuua bila kukusudia inayowakabili wamiliki watatu wa jengo lililoporomoka Mtaa wa Mchikichi na Congo, eneo la Kariakoo, itatajwa leo Desemba 12, 2024 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Washtakiwa katika kesi hiyo, ambao wote ni wakazi wa Dar es Salaam ni Leondela Mdete (49) mkazi wa Mbezi Beach, Zenabu Islam (61) mkazi wa Kariakoo na Ashour Awadh Ashour (38) mkazi wa Ilala.
Mdete na wenzake wanakabiliwa na mashtaka 31 ya kuua bila kukusudia, katika mahakama hiyo.
Kesi hiyo imepangwa kutajwa leo mahakamani hapo na kuangalia iwapo upelelezi wa shauri hilo umekamilika au la.
Pia, Soma