Kesi ya Jerry Muro yarudi tena kortini

Kesi ya Jerry Muro yarudi tena kortini

kabanga

JF-Expert Member
Joined
Dec 12, 2011
Posts
37,421
Reaction score
18,760
UPANDE wa Mashitaka katika rufaa ya kupinga kuachiwa huru kwa Aliyekuwa Mtangazaji wa Shirika la Utangazaji (TBC) Jerry Murro aliyekuwa anakabiliwa na mashitaka ya kuomba rushwa ya Sh milioni 10 umeiomba Mahakama Kuu Kanda ya Dar es salaam kuamuru kesi hiyo isikilizwe upya.

Mawakili wa wa Serikali walidai hayo jana mbele ya Jaji Fauz Twaib kwa kuwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ilikosea kisheria katika kuweka kumbukumbu ya Mwenendo wa
kesi hiyo jambo lililosababisha kutoa uamuzi usio wa haki.

Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP), Dk Eliezer Feleshi alikata rufaa kupinga hukumu iliyotolewa Novemba 30 mwaka juzi na Hakimu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Frank Moshi, ambayo ilimuachilia huru Murro, Deogratius Mgasa na Edmund Kapama waliokuwa wanakabiliwa na mashitaka hayo.

Katika rufaa hiyo, Wakili wa Serikali Awamu Mbagwa alidai kuwa mahakama haikuandika vizuri kumbukumbu za ushahidi na vielelezo katika Mwenendo wa kesi ambapo kuna baadhi ya
ushahidi haueleweki unamaanisha nini jambo lililosababisha Hakimu kufikia uamuzi usio wa haki.

Aidha alidai kuwa kuna baadhi ya vielelezo na ushahidi haupo kwenye mwenendo wa kesi, ikiwemo maelezo ya onyo yaliyotolewa na Murro katika kituo cha polisi na kitabu cha wageni waliofika katika hoteli ya Sea Cliff ambayo wajibu rufaa wanadaiwa kuomba rushwa.

Aliieleza mahakama kuwa, kitabu cha wageni kilikataliwa kupokelewa mahakamani kama kielelezo lakini katika Mwenendo wa kesi haijaandikwa na hata uamuzi wa pingamizi la kielelezo hicho haukutolewa na kudai kuwa kukosekana kwa uamuzi huo kumesababisha Hakimu kutofikia uamuzi wa haki.

Aidha katika mwenendo wa kesi hakuna kumbukumbu za wao kuwasilisha Mkanda wa kamera inayonasa matukio (CCTV) ulioonesha wajibu rufaa walipokwenda kufanya
makubaliano ya kupokea rushwa, lakini walishindwa kuuangalia na baadaye wakaamua kutumia picha za kawaida.

Aliongeza kuwa kesi hiyo awali ilikuwa inasilizwa na Hakimu Gabriel Mirunde lakini Hakimu Frank Moshi ndiye aliyetoa hukumu hivyo kutokana na kuandikwa vibaya kwa mwenendo wa kesi hiyo Hakimu Moshi alishindwa kuelewa ushahidi na utoa uamuzi usio wa haki.

Akijibu hoja wakili wa Murro, Richard Rweyongeza aliiomba mahakama kutupilia mbali hoja hiyo kwa uwa haina misingi kisheria pia wakata rufaa hawajaeleza ni vipi kukosewa kwa mwenendo wa kesi hiyo kumesababisha kufikia uamuzi usi sahihi.

Naye Wakili wa wajibu rufaa wengine, Majura Magafu alidai kuwa wakata rufaa hawajalalamika kuhusu hukumu iliyotolewa bali maandishi katika mwenendo wa kesi na katika hukumu hiyo hakuna sehemu ambayo Hakimu alilalamika kuwa alipata shida kusoma mwenendo wa kesi hiyo.

Alidai endapo mahakama itamua kesi hiyo isikilizwe upya itakuwa ni sawa na kufanyabiashara ya kuchagua mahakimu kuwa kama wameshindwa kwa hakimu huyo wajaribu kwa mwingine jambo ambalo haliruhusiwi kisheria.

Warufani walikuwa na sababu nne lakini imesikilizwa sababu moja ambapo baada ya kusikiliza hoja hizo Jaji Twaib aliahirisha shauri hilo hadi Aprili 29 mwaka huu atakapotoa uamuzi.

Washitakiwa wanadaiwa kuwa waliomba rushwa kutoka kwa aliyekuwa Mhasibu wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo, Michael Wage kwa lengo la kuzuia kutangazwa kwenye
televisheni habari za tuhuma za ubadhirifu wa fedha za umma akiwa mhasibu wa halmashauri hiyo.

Katika madai hayo, Muro na wenzake wanadaiwa Januari 28 mwaka jana jijini Dar es Salaam, walikula njama ya kutenda kosa hilo na Januari 29 mwaka jana katika Hoteli ya
Sea Cliff Dar es Salaam waliomba rushwa ya Sh milioni 10 kutoka kwa Wage.
 
Hivi wale wahasibu wa huko Bwagamoyo waliokula pesa za halmashauri zaidi ya Milioni mia waliishia wapi au ndo Muro alikamatwa kuua soo la wale wahasibu. Nchi hii bana kila kitu kinaenda kinyume nyume
 
UPANDE wa Mashitaka katika rufaa ya kupinga kuachiwa huru kwa Aliyekuwa Mtangazaji wa Shirika la Utangazaji (TBC) Jerry Murro aliyekuwa anakabiliwa na mashitaka ya kuomba rushwa ya Sh milioni 10 umeiomba Mahakama Kuu Kanda ya Dar es salaam kuamuru kesi hiyo isikilizwe upya.

Mawakili wa wa Serikali walidai hayo jana mbele ya Jaji Fauz Twaib kwa kuwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ilikosea kisheria katika kuweka kumbukumbu ya Mwenendo wa kesi hiyo jambo lililosababisha kutoa uamuzi usio wa haki. Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP), Dk Eliezer Feleshi alikata rufaa kupinga hukumu iliyotolewa Novemba 30 mwaka juzi na Hakimu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Frank Moshi, ambayo ilimuachilia huru Murro, Deogratius Mgasa na Edmund Kapama waliokuwa wanakabiliwa na mashitaka hayo.

Katika rufaa hiyo, Wakili wa Serikali Awamu Mbagwa alidai kuwa mahakama haikuandika vizuri kumbukumbu za ushahidi na vielelezo katika Mwenendo wa kesi ambapo kuna baadhi ya ushahidi haueleweki unamaanisha nini jambo lililosababisha Hakimu kufikia uamuzi usio wa haki.

Aidha alidai kuwa kuna baadhi ya vielelezo na ushahidi haupo kwenye mwenendo wa kesi, ikiwemo maelezo ya onyo yaliyotolewa na Murro katika kituo cha polisi na kitabu cha wageni waliofika katika hoteli ya Sea Cliff ambayo wajibu rufaa wanadaiwa kuomba rushwa. Aliieleza mahakama kuwa, kitabu cha wageni kilikataliwa kupokelewa mahakamani kama kielelezo lakini katika Mwenendo wa kesi haijaandikwa na hata uamuzi wa pingamizi la kielelezo hicho haukutolewa na kudai kuwa kukosekana kwa uamuzi huo kumesababisha Hakimu kutofikia uamuzi wa haki.

Aidha katika mwenendo wa kesi hakuna kumbukumbu za wao kuwasilisha Mkanda wa kamera inayonasa matukio (CCTV) ulioonesha wajibu rufaa walipokwenda kufanya makubaliano ya kupokea rushwa, lakini walishindwa kuuangalia na baadaye wakaamua kutumia picha za kawaida. Aliongeza kuwa kesi hiyo awali ilikuwa inasilizwa na Hakimu Gabriel Mirunde lakini Hakimu Frank Moshi ndiye aliyetoa hukumu hivyo kutokana na kuandikwa vibaya kwa mwenendo wa kesi hiyo Hakimu Moshi alishindwa kuelewa ushahidi na utoa uamuzi usio wa haki.

Akijibu hoja wakili wa Murro, Richard Rweyongeza aliiomba mahakama kutupilia mbali hoja hiyo kwa uwa haina misingi kisheria pia wakata rufaa hawajaeleza ni vipi kukosewa kwa mwenendo wa kesi hiyo kumesababisha kufikia uamuzi usi sahihi. Naye Wakili wa wajibu rufaa wengine, Majura Magafu alidai kuwa wakata rufaa hawajalalamika kuhusu hukumu iliyotolewa bali maandishi katika mwenendo wa kesi na katika hukumu hiyo hakuna sehemu ambayo Hakimu alilalamika kuwa alipata shida kusoma mwenendo wa kesi hiyo. Alidai endapo mahakama itamua kesi hiyo isikilizwe upya itakuwa ni sawa na kufanyabiashara ya kuchagua mahakimu kuwa kama wameshindwa kwa hakimu huyo wajaribu kwa mwingine jambo ambalo haliruhusiwi kisheria.

Warufani walikuwa na sababu nne lakini imesikilizwa sababu moja ambapo baada ya kusikiliza hoja hizo Jaji Twaib aliahirisha shauri hilo hadi Aprili 29 mwaka huu atakapotoa uamuzi. Washitakiwa wanadaiwa kuwa waliomba rushwa kutoka kwa aliyekuwa Mhasibu wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo, Michael Wage kwa lengo la kuzuia kutangazwa kwenye televisheni habari za tuhuma za ubadhirifu wa fedha za umma akiwa mhasibu wa halmashauri hiyo.

Katika madai hayo, Muro na wenzake wanadaiwa Januari 28 mwaka jana jijini Dar es Salaam, walikula njama ya kutenda kosa hilo na Januari 29 mwaka jana katika Hoteli ya Sea Cliff Dar es Salaam waliomba rushwa ya Sh milioni 10 kutoka kwa Wage.

SOURCE: MAJIRA
 
Jerry alikua anapinga rushwa, jeshi la polisi likamtungia kesi hii.
Hakika ukiwa mpinga rushwa unapata maadui wengi sana hapa tanzania.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Jerry alikua anapinga rushwa, jeshi la polisi likamtungia kesi hii.
Hakika ukiwa mpinga rushwa unapata maadui wengi sana hapa tanzania.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
Si nasikia walimrecord wakati yeye anapokea rushwa, na alikuwa na pingu kama yeye ni polisi?
 
Si nasikia walimrecord wakati yeye anapokea rushwa, na alikuwa na pingu kama yeye ni polisi?

kama walimrekodi walipaswa kushinda kesi ya awali, mbona ushaidi huo haukufanikiwa?
izo picha zilitengenezwa na masha(waziri wa zamani) na mahakama iligundua kuwa ni magumashi.

Kuhusu pingu muro aliwashinda kwasababu kwenye sheria zetu hakuna aliyekatazwa kumiliki pingu.
 
si wamfunge basi, mbona wanamwachia. yeye naye pingu zilikuwa za nini? masilaha kama jeshi la familia? simtetei
 
Kesi ya Jerry Muro imeanza upyaa, na safari hii inasemekana haponi kabisa. lazima apigwe kitanzi. Nasikia anatamba kwa watu kuwa, aliyekuwa anamheshimu na kumuona kama atamtia kitanzi ni marehemu Bon aliyekuwa anaendesha kesi yake, huyo boni ameshakufa, lakini taasisi ya waendesha mashitaka haijafa, wapo wengine wataungana kumshitaki. inasemekana kuna kikundi kikubwa cha mawakili (sina uhakika lakini) watakaotoka mikoani wote waje washambulie hii kesi ya Muro. Kachelo wetu wa polisi alihudhuria mahakamani juzi, inasemekana muro wa kipindi kile sio muro wa kipindi hiki, amenywea ile mbaya. kiburi chake cha kutangaza ndoa kabla ya hukumu kitaisha kwasababu ataspend miaka kadhaa ndani na nje mkewe akiwa peke yake bila kupata haki yake ya unyumba....kama anaweza, amtie mkewe mimba haraka kwasababu akichelewa ataenda ndani na akitoka gerezani anaweza kuja kukuta mkewe ana watoto hata wawili wa mwanaume mwingine.
 
Mbona hii thread imekaa kiunafiki sana??wewe ni mhusika??
 
Kesi ya Jerry Muro imeanza upyaa, na safari hii inasemekana haponi kabisa. lazima apigwe kitanzi. Nasikia anatamba kwa watu kuwa, aliyekuwa anamheshimu na kumuona kama atamtia kitanzi ni marehemu Bon aliyekuwa anaendesha kesi yake, huyo boni ameshakufa, lakini taasisi ya waendesha mashitaka haijafa, wapo wengine wataungana kumshitaki. inasemekana kuna kikundi kikubwa cha mawakili (sina uhakika lakini) watakaotoka mikoani wote waje washambulie hii kesi ya Muro. Kachelo wetu wa polisi alihudhuria mahakamani juzi, inasemekana muro wa kipindi kile sio muro wa kipindi hiki, amenywea ile mbaya. kiburi chake cha kutangaza ndoa kabla ya hukumu kitaisha kwasababu ataspend miaka kadhaa ndani na nje mkewe akiwa peke yake bila kupata haki yake ya unyumba....kama anaweza, amtie mkewe mimba haraka kwasababu akichelewa ataenda ndani na akitoka gerezani anaweza kuja kukuta mkewe ana watoto hata wawili wa mwanaume mwingine.

Huna hoja...una chuki binafsi na Jerry au mkewe! Get over it, the dude won the case...plus married a beautiful wife who stood by him through that tough time!
 
Mmmmh hiii kesi? Usishangae kuna mkono wa baba hapo...hao wahasibu kwann wajiamin hvyo..maana yke wahasibu n njia tu mwenyew yupo
 
Wanahangaika na kesi za kuungaunga wkt midude yenye nywele nyeupe imepunzika bungeni
 
nina chuki naye ndiyo, kwasababu jamaa ni mnafiki sana. kuna siku wale wanasheria watamuweka ndani, mkewe akiwa nje nitamlamba hadi mimba. alijifanya anapiga watu picha za rushwa kumbe na yeye ni mla rushwa.
 
nina chuki naye ndiyo, kwasababu jamaa ni mnafiki sana. kuna siku wale wanasheria watamuweka ndani, mkewe akiwa nje nitamlamba hadi mimba. alijifanya anapiga watu picha za rushwa kumbe na yeye ni mla rushwa.

Alaa sasa kama unachuki zako sasa hapa unataka kutuaminisha chuki sisi za kazi gani? Kwani huna namba yake ukampigia?
 
Back
Top Bottom