sammosses
JF-Expert Member
- Jan 24, 2011
- 1,687
- 1,111
Wakuu,
Ndani ya JF tunanufaika na elimu nyingi ili kutuweka sawa Watanzania na kuishi kwa kujiamini pasi na kuvunja sheria,imekuwa ni jambo la kawaida ndani ya nchi yetu wananchi kunyanyasika sana kutokana na kutokujua sheria japokuwa kuna msemo wa kisheria usemao kutokujua sheria si sababu ya kuvunja sheria.
Leo nataka nizungumzia mabadiliko ya kisheria yanayofanywa na serikali ndani ya bunge letu tukufu ambayo sheria hizo zinachelewa kutumika na kupelekea wananchi kunyanyasika kwa kutokujua ilihali rais wa nchi ameshasaini repeal ya sheria zilizopitwa ili kuweza kutumika kwa sheria mpya.Mimi si mwanasheria kitaalumaa ila nilitaka kujua ikiwezekana kufungua kesi ya kikatiba ambayo inasababishwa na serikali kutozitumia sheria zilizosainiwa na rais kutumika kwa kigezo cha kutokutungiwa regulation zake.
Ningependa wataalamu wa sheria mniweke sawa kidogo ili niweze kupata mwanga wa kisheria kutokana na sheria ambazo zimetungwa toka mwaka 2008 lakini mpaka leo hii zimekuwa hazitumiki kutokana tu na kutokuwa na kanuni kitendo kinachopelekea wananchi kukosa haki zao za msingi.
Mathalani kuna sheria ya hotel and tourism act ambayo rais alisaini repeal ya sheria ya mwaka 2006,nikiwa na maana kama sheria ilishafutwa na kusainiwa sheria mpya kuna haja gani ya kuendelea kuitumia sheria ya zamani ilhali ilishafutwa ama kwa kuonekana kandamizi au haikukidhi hali ya wakati uliopo.Nani hasa ambaye ana takiwa kusimama kujibu hoja ikiwa waziri na wataalamu wake wameshindwa kutunga regulation na kusababisha wananchi kuendelea kukandamizwa kwa kutumia sheria ya zamani.
Jambo la Pili nikutaka kujua ni duration gani ambayo inataka sheria ianze kutumika mara baada ya rais kuisani kutumika hata kama haijatungiwa regulation zake.Pia nini cha kufanya ikibainika kuna sheria ambazo hazijaanza kutumika kwa makusudi ili kuwakomoa Watanzania kwakuwa tu ni mbumbumbu wa sheria.[/CODE]