Kesi ya kubambikiwa ya Susana binti Hilkia

Kesi ya kubambikiwa ya Susana binti Hilkia

BAK

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2007
Posts
124,790
Reaction score
288,165
Wakuu (viongozi) wawili katika Israeli ya Kale waliamua kumbambikia Kesi Susana Binti Hilkia kwa sababu aliwakatalia mambo yao. Waliamua kumburuza Mahakamani ambako walitoa ushahidi wa uongo na Susana akahukumiwa kunyongwa hadi kufa.

Kiongozi wa Mawakili wa Upande wa Utetezi, Wakili Msomi Danieli alikata rufaa katika Mahakama ya Rufani. Hebu sikiliza alipokuwa akiwapelekesha kwa maswali Mashahidi wa Upande wa Mashitaka:

Wakili Msomi Danieli: Shihidi! Wewe mtu muovu! Uovu wako wa siku nyingi leo ndio unafikia ukomo! Umezoea kutoa hukumu isiyo ya haki, ukiwatuhumu na kuwaonea watu wema na kuwapendelea waovu ingawa Mungu amesema msiwaue watu wasio na makosa!

Jaji: Endelea kumhoji Shahidi, Ee Wakili Msomi Danieli

Wakili Msomi Danieli: Shihidi: Sasa nakutaka unieleze mimi na Mahakama hii! Ni katika mti upi ambapo ulimuona mshitakiwa Susana akitenda uovu huo?

Shahidi wa Kwanza: Katika mti wa mkarafuu!

Wakili Msomi Danieli: Sawa sawa! Uwongo wako utayagharimu maisha yako! Tayari Malaika wa Bwana amepokea hukumu yako!

Jaji: Mleteni Shahidi wa Pili ili naye ahojiwe na Wakili Msomi Danieli wa Upande wa Utetezi

Wakili Msomi Danieli: (anamkazia macho) Shahidi! Tunajua jinsi ambavyo umekuwa ukiwanyanyasa wanawake katika nchi hii! Hapa kuna mwanamke (Susana) ambaye hakutaka kuburuzwa na wala hakuogopa vitisho vyako!

Jaji: Endelea kumhoji Shahidi wa Pili, ee Wakili Msomi Danieli

Wakili Msomi Danieli: Nieleze mimi pamoja na Mahakama hii! Ni katika mti gani ulimkuta Susana akitenda uovu huo?

Shahidi wa Pili: Katika mti wa Mbuyu!

Wakili Msomi Danieli: Sawa kabisa! Uwongo wako utakugharimu maisha yako. Tazama! Malaika wa Bwana amepokea hukumu yako!

Umati wa watu: Haleluya! Haleluya! Haleluya! [Haleluya maana yake ni msifuni Mungu]

Jaji: Upande wa Mashitaka umeshindwa kuthibitisha pasipo mashaka kuhusu tuhuma za mshitakiwa, hivyo Mahakama hiii inamuachia huru Susana Binti Hilkia. Mahakama inawatia hatiani Mashahidi wawili upande wa Mashitaka na kuwahukumu kifo kwa kushuhudia uwongo mbele ya Mahakama.

NB: Ukitata kusoma vizuri Kesi hiyo, soma kitabu cha Danieli na Susana. Kitabu hiki kina Sura moja tu yenye mistari 64. Ni sehemu ya vitabu vya Apocrypha ambavyo havijawa sehemu ya Biblia katika baadhi ya madhehebu ya Kikristo lakini kinatumiwa kama rejea ya hekima na mabingwa wa theologia. Sisi Askofu tumeweka Habari ya Susana katika mfumo wa Kimahakama za kisasa ili kurahisisha uelewa!

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula
 
Hadithi hii ya kubumba na anayejiita askofu bila kuwekwa wakfu inatufundisha nini? Mbowe
 
Back
Top Bottom