Mkalukungone mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 862
- 1,755
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kivukoni, iliyoko Kinondoni, imeshindwa kuanza usikilizwaji wa kesi ya kumjeruhi na kutishia kwa silaha ya moto (bastola), katika klabu ya usiku (Night Club) 1245, Masaki, Dar es Salaam, kutokana na mlalamikaji kuchelewa kufika mahakamani kwa muda uliopangwa.
Katika kesi hiyo, mshtakiwa Derick Derick Junior (36), mkazi wa Salasala, jijini Dar es Salaam, anakabiliwa na mashtaka mawili: kujeruhi na kutembea na silaha hadharani kwa namna ya kuleta utisho.
Anadaiwa kutenda makosa hayo Oktoba 27, saa 12:30 asubuhi, katika Kklsbu hiyo, eneo la Masaki wilayani Kinondoni.
Soma Pia: Kesi ya Mtumishi wa TRA aliyetishia Bastola na kujeruhi mtu Club 1245 yapigwa Kalenda hadi Januari 21, 2024
Kesi hiyo inayosikilizwa na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa mahakama hiyo, Is-haq Kuppa, ilitarajiwa kuanza kuunguruma leo rasmi, kwa Mahakama kuanza kupokea ushahidi wa upande wa mashtaka.
Hata hivyo, usikilizwaji hakufanyika kutokana na mlalamikaji, Bujuru, ambaye ni shahidi wa kwanza wa upande wa mashtaka, aliyetarajiwa kuanza kutoa ushahidi wake, kuchelewa kufika mahakamani kwa muda uliopangwa.