Kesi ya kumtukana mtu kwa ujumbe wa simu(sms)

Yohana Kilimba

JF-Expert Member
Joined
Dec 25, 2012
Posts
8,105
Reaction score
5,629
Naomba kuuliza na kusaidiwa:
a)kuna rafiki yangu amesingiziwa kumtukana shemeji yake kwa ujumbe wa simu(sms)
b)alipoenda polisi,na kuandika jalada,polisi wakachukua simu zake mbili kama ushaidi
c)baada ya miezi polisi miwili wakairudisha moja wakabaki na moja
d)kesi ikaenda mahakama ya mwanzo na jamaa akakana kosa,na kama ushaidi polisi wakaileta ile simu
e)na baada ya kujitetea hakimu akusikiliza ushaidi wa mshitakiwa
f)tarehe ya hukumu ishapangwa(09-07-2015)
g)naomba kujua jamaa atahukumiwa kwa sheria hipi na kanuni zipi?ili tuandae rufaa
 
Nenda kwa maconsultancy wa sheria wakupe ushauri muafaka
 
Subiri tu atapewa fine elfu kumi basi. Ndo tanzania hiyo
 
Subiri hukumu itoke kwani umeshajua kuwa ametiwa hatiani au laaa.

Na unaposema kuwa mshitakiwa hajapewa nafasi ya kujitetea kivipi? Una uhakika na hicho unachosema? Labda km hivyo ndivyo basi sio hukumu bali ni uamuzi wa kujua km mshitakiwa anakesi ya kujibu au las.

Endapo atakutwa na kesi ya kujibu ndipo hapo atakapopewa nafasi ya kujieleza na kuleta ushahidi wake na baadae hukumu ndo itatoka

Endapo ataonekana hana kesi ya kujibu, basi ataachiliwa.
Ila hiko ulichosema kuwa ipo hivyo sikiamini kabisa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…