Kesi ya kupinga tozo za miamala kutajwa Mahakamani leo Agosti 16, 2021

Kesi ya kupinga tozo za miamala kutajwa Mahakamani leo Agosti 16, 2021

mshale21

JF-Expert Member
Joined
Apr 8, 2021
Posts
2,126
Reaction score
5,068
Kesi ya kupinga tozo za miamala ya simu iliyofunguliwa na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) leo Agosti 16, 2021, itatajwa tena kwa mara ya pili katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Anna Henga

Taarifa ya kesi hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Anna Henga, na kueleza kuwa kesi hiyo ilifunguliwa Julai 27 mwaka huu.

Tozo ya uzalendo katika miamala ya simu kwa mtumaji ama mpokeaji wa pesa zilianza kutozwa Julai 15 mwaka huu, na tayari serikali iliahidi kulishughulikia suala hilo baada ya kupokea malalamiko mengi kutoka kwa wananchi.
 
Mbuzi afia kwa Mgongo wa fisi, sizan kama hiyo kesi itashinda kwa upande wa watetezi wa wananchi, maana hawa c+c+m na mama yao wamesema tumekubali huo ukaghai wao, na wameshaupitisha, hivo tegemeeni mabadiriko 0" ....
 
Tena hao waliofungua kesi inatakiwa wakamatwe na niwahujumu uchumi,mbona sisi wananchi tumeshakubali na tumesema inatakiwa tozo iongezwe iwe nusu kwa nusu,
we ni mdudu tu umekubali na nani sema Mimi nimekubali
 
Hii case itaungwa mkono na wanyonge wote, hata waliombishia Magufuli kuwa wao siyo.
 
Pongezi[emoji122][emoji122][emoji122]
 
Hao LHRC wanatukwamisha kupata maendeleo vijijini.
Wanadhani maendeleo kama Ya Magufuri tutayafikiaje bila hizo Tozo?
 
Back
Top Bottom