Kesi ya kushindwa kutunza kumbukumbu za dereva, naomba msaada

Muntu Ya Pori

JF-Expert Member
Joined
Jun 25, 2013
Posts
222
Reaction score
64
Habari zenu wakuu.

Natuhumiwa na kesi ya kutotunza kumbukumbu za dereva. Mambo yalikua hivi, tarehe 8/6/2014 jamaa alichukua pikipiki yangu kwa ajiri ya shughuli zake binafsi huwa namuazima kila anapohitaji,siku hiyo kaenda kapakia watu wawili na kupata ajari kubwa tu dereva,abiria na pikipiki hali mbaya. Walichukuliwa wote na kupelekwa hospital. Baada ya siku mbili dereva aliruhusiwa kutoka hospital na kurejea kwake. Abiria mmjoja hakuumia ila mwingine ilipelekea kukatwa mguu kabisa.

Nilijaribu kufuatilia jinsi ya kuitoa pikipiki yangu, siku ya kwanza nilienda peke yangu wakasema wanataka maelezo ya dereva. Nilimwambia huyo dereva sasa siku anaenda hakumkuta muhusika aliyekua anasimamia hilo suala aliishia kupewa namba zake tu.

Tulijaribu kupiga namba hizo, kuna wakati haipatikani au inaita bila kupokelewa. Mi nikasema nitafuatilia siku nikipata nafasi maana nafanya kazi private so muda wa kiwepo kazini ni muhimu sana. Kulikuwa na likizo mwezi wa saba mi nikasafiri kuwatembelea ndugu na jamaa. Nilipo rudi nilikuta dereva nae kaenda kusalimia kwao(mkoani).

Nikaenda tena kituoni na kumuelezea hali ilivyo kwa sababu walitaka maelezo ya dereva na dereva kasafiri itakuaje. Jamaa aliniambie niende na vielelezo vinavyothibiti umiliki wa pikipiki, nikaenda kituoni sikumkuta nilipowasiliana nae kaniambia wako busy kamatakamata. Nikatulia kufuatilia. Nilipoteza contact za huyo trafic.

Tarehe 6/8/2014 nilipata nafasi kikazi kwenda posta nilipokuwa narudi nikaamua nipitie kituoni nimuone trafic muhusika nijue natoa vipi pikipiki yangu. Nilipofika kituoni sikumkuta akibiti nichukue namba yake kwa mkuu wake.

Nilipompigia akaniambia katoka ila nimsubiri, alipokuja ndo kaandika kesi tajwa hapo juu na kuniweka ndani kusubiri uamuzi wa mahakama. Nipo nje kwa dhamana. Samahani kwa maelezo mengi. Naomba msaada kwa hilo jtatu nasimama mahakamani

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
 
pole mkuu, usiogope Mungu yupo upande wako

naamini wapo wanasheria humu ndani watakusaidia lakini pia ni muhimu pia ww ikajiandaa mwenyewe ikiwa nikutafuta msaada wa kisheria na wakili usije ukakwamishwa shughuli zako muhimu kwa kusudi lakupangwa.
 
Ila mkuu haujaeleza unataka msaada wa nini ili usaidiwe.!!
 
Ila mkuu haujaeleza unataka msaada wa nini ili usaidiwe.!!

Ni jinsi gani naweza kutatua hii issue.jinsi gani naweza kuwa free from hili jambo.

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
 
Mkuu kwakua uko nje kwa dhamana hopefully,wamekueleza tarehe ya kwenda mahakamani,kwa hapo polisi akuna cha maana utakachoweza kusaidiwa may b kama utataka kuwapa rushwa mambo yaishe hapo kitu ambacho si kizuri,subiria uende mahakamani usomewe mashitaka yako then tuanzie hapo tuona tutasaidiana vipi..mimi ni hayo tu..
 

Poa mkuu. Jtatu ndo tunaenda mahakamani. Nitawajuza yatokanayo. Asante kwa kujari mkuu!

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
 
Hakikisha unaenda na mtu wa kukudhamini mahakani maana dhamana ya polisi itakoma Jumatatu baada ya kusimama kizimbani. Chukua barua kwa Mtendaji wako.
 
Mwanasheria bado hajaandaa jarada la mashitaka so wameniambie niende jtano.

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…