Haha!! Issue hii imeonyesha wazi kuwa 99% ya wana JF hawako makini katika uchambuzi wao. Ni only 1% waliosema kuwa tusubiri mpaka leo 24/02 ndio tujue hatma ya jambo hili ndio waliopatia na ndio waliokuwa na mchango wa busara.
Imagine sisi wengine tulisema mambo kibao na kuwatukana watu na serikali bila kuwa na subira. Maneno yetu yote yameishia kapuni. wahenga walisema "time is the greatest healer"
Kwanza unasema 99% ya wana JF sijui ni formula gani hio uliyotumia...Ila karibu JF na utaendelea kujifunza tu.
Pili naomba nikukumbushe kitu kimoja;Kwenye data processing kuna Input Proceesing Output (IPO mode)Mwakatojofu amegusia baadhi ya points hapo juu na mimi nita add just a couple...
1)Masharti ya mdhamana yalikiukwa kwa vielelezo visivyokidhi mahitaji ya mdhamana na hivyo wachambuzi wa mambo lazima watahoji...This is regardless of the fact kuwa bail money ilikuwa reduced kwa kwa namna ambayo inazua maswali.
2)Mahakama iliwashikilia kwa muda wadhamini kwani mtuhumiwa hakufika mahakamani hapo ambapo aliitwa kabla ya tarehe hiyo feb 24 ambayo kila mtu alijuwa ndio siku kesi itakapotajwa tena except sababu ya kuitwa mahakamani kabla ya siku ya kesi ndiyo hakuna anayejuwa ila tulidhani kuwa ni kwasababu ya fununu kuwa litoroka na mazingira ya document zake un qualified.(rejea kauli ya hakimu Khadija kwamba faili liko mahakama kuu)
3)TAKUKURU wakatangaza "donge nono" kwa mwenye taarifa za kuwezesha kupatikana kwa mtuhumiwa.....Hapo tukajuwa ni kweli mtuhumiwa hapatikani...Sasa TAKUKURU wenyewe wako hapo bongo na wakakiri katoroka..Sisi je? Mazingira yote ya kesi yalipelekea mjadala huu kuenda ulivyoenda...Kwa maana kwamba ni input ya data hapa JF na tukaprocess na information ndio kama ilivyo kama unavyosikia huko mahakamani mvutano kuhusu mdhamana na documents....Hatukuanzisha hizi habari ila sisi tulikuwa tuna process ama tuna analyze,all in all hata kama walikuwa wanapima zali wamegunduwa mboga moto na ugali moto kama nilivyosema huko nyuma.
Kwa kifupi ni kwamba huwezi kukaa pembeni halafu unakuja mwishoni na kudai eti ilikuwa mseme hivi na si vile kwasababu tulikuwa wrong, na mambo ya 1% ya JF na 99% ambayo hata namna uliyofikia hiyo conclusion haujulikani,kwamba eti busara,haa hii ndio busara...If that was the case JF isingekuwa hapa JF mkuu....Na kwamba eti habari ikija sijui hatufahamu kama ni kweli...Mambo haya na mawazo haya sishangazwi kwani hata Pengo na yeye ana mawazo kama yako tu...Sasa na habari za Ufisadi zilianzia wapi? Si ziliitwa porojo za vyombo vya habari na mtandao?
Ndugu tk quit be an opportunist na uchangie mjadala si kwa madhumuni ya kushindana bali kuelimishana.
Na pia unaposema tuliwatukana watu wa serikalini bila subira, kwani TAKUKURU ni ya wapi? Mahakama ni ya wapi? Kwenda mahakamani kwa Liyumba haina maana kuwa serikali haikufanya makosa, na ndio maana kama ulifuatilia mjadala huu nilisema kuwa tusijadili sana kuhusu kutoroka bali tujadili kuhusu mazingira ya mdhamana wake kwasababu bottomline lazima kuwe na accountability, kutokuja bila escort ni kujaribu kuwasifisha waliokuwa responsible,kwamba hakukuwa na nia yoyote ya kumtorosha,kama kulikuwa na mawasiliano mabovu kiasi cha TAKUKURU kutangaza pesa kwa mtuhumiwa aliyetoroka basi JF tulikuwa na haki ya kusema lolote.