Kesi ya maadili inayowakabili Ali Kamwe na Ahmedy Ally yasogezwa mbele na TFF

Kesi ya maadili inayowakabili Ali Kamwe na Ahmedy Ally yasogezwa mbele na TFF

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Kesi ya Ahmed Ally na Ally Kamwe iliyowapeleka kuitwa kamati ya Maadili ya shirikisho la mpira wa miguu nchini (TFF) imepelekwa mbele mpaka hapo kesho.

===

Mapema leo, Mameneja hao wa Habari na Mawasiliano wa vilabu vya Simba Sc na Yanga Sc, Ahmed Ally na Ally Kamwe wote wameitwa kwenye Kamati ya Maadili ya Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) kwa tuhuma za kutenda makosa ya kimaadili.

Wawili hao wameripoti asubuhi ya leo, Machi 3, 2025 kwenye ofisi za TFF zilizopo Karume, Dar es Salaam kwaajili ya kusikiliza kusomewa makosa yao na hukumu.

Haya yanajiri zikiwa zimesalia siku tano tu kabla ya wawili hao kukumbwa na joto la Derby ya Kariakoo, pale wenyeji, Yanga Sc watakapochuana na Simba Sc katika dimba la Benjamin Mkapa siku ya Jumamosi, Machi 8, 2025.
 
Wacambuzi/ wachambaji wa Tanzania ni wapuuzi sana. Unakuta mtu badala ya kumhoji mtu wa technical anamhoji afisa habar juu ya jambo technical?
Mwisho wa siku wanakosa habar na kubwabwaja ujinga
 
Wacambuzi/ wachambaji wa Tanzania ni wapuuzi sana. Unakuta mtu badala ya kumhoji mtu wa technical anamhoji afisa habar juu ya jambo technical?
Mwisho wa siku wanakosa habar na kubwabwaja ujinga
Yaani wanakuwa na akili ya kuhoji Mambo mengine lakini la marefa wanao boronga uwanjani hizo akili zinakuwa hazipo
 
Back
Top Bottom