Kesi ya madai 10m nimlipeje wakili aliyeisimamia?

MAGUNJA

JF-Expert Member
Joined
Jul 3, 2012
Posts
1,003
Reaction score
545
Ndugu wadau naomba mnishauri nina kesi ya madai ya milioni 10. Je wakili anayenisimamia nitamlipa shilingi ngapi? Au kuna malipo fixed yasiyojali madai ni ya kiasi gani?
Naomba kuelimishwa.
 
elewana nae au kwa lugha nyingine bargain nae
 
kumbuka unamwajiri wakili akufanyie kazi yako 'kwa uwezo wake wote'. kama akijua hakulipwa vizuri, hatokuwa na morali ya kuifanya kazi yako kwa moyo wake wote. na hapo inaweza kula kwako, manake hutoweza kujua kama kazi yako kaifanya kwa uwezo wake wote au kabangaiza kiaina. vitu vingine ni binafsi na kumlalia mtu kama huyo hakusaidii kesi yako
 
Reactions: Obe
Ndugu uwakili unaendeshwa kwa sheria na sheria hiyo inatoa nafasi kwa mteja na wakili kukubaliana katika malipo, kuna kesi zinaitwa contentious cases na non-contentious, kwa hii non kuna prescribed scale za kumlipa wakili na kwa kiasi kama chako (kama ni non-contentious) ni asilimia 3% ila wakili abanwi na hii asilimia, na kama ni cont...ni maelewano yako na wakili wako na hii inatofautiana kwa mawakili wote!
 
Thank u wadau. You have opened my eyes at least I have where to start.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…