WomanOfSubstance
JF-Expert Member
- May 30, 2008
- 5,457
- 963
RAIS Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa, anatarajiwa kupanda kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Mei 8, mwaka huu kumtetea aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Italia, Profesa Costa Mahalu.Wakili anayemtetea Balozi Mahalu, Mabere Marando alisema jana kwamba Mkapa atapanda kizimbani siku moja baada ya Profesa Mahalu kumaliza kutoa utetezi wake.
Awali, akizungumza mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Ilvin Mgeta Wakili Marando alisema Mei 8, kutakuwa na shahidi mwingine wa mwisho muhimu ambaye hata hivyo, hakumtaja.
Alipoulizwa kuhusu shahidi huyo nje ya Mahakama, Marando alimtaja kuwa ni Rais Mstaafu Mkapa na baadaye alipopigiwa simu kutoa ufafanuzi zaidi alisema: Mkapa ni shahidi wa Mahalu hivyo atafika mahakamani kutoa ushahidi wake kwa maneno. Source :http://www.mwananchi.co.tz/componen.../22523-kesi-ya-mahalumkapa-kortini-mei-8.html
Swali ni je, Mkapa akikubali kwenda "kutoa ushahidi kwa kumtetea Mahalu", haitamweka pabaya kwamba anaweza kujikuta akitakiwa mahakamani kwa kesi mbalimbali maana kuna mlolongo wa mashauri yanayotokana na watendaji wa kipindi chake kukiuka sheria mbalimbali.
Wanasheria hebu nongesheni mjadala huu kwa kuzingatia zaidi SHERIA na SIYO SIASA.