Kesi ya Masheikh; Mahakama ya Rufaa yatupilia mbali rufaa ya Jamhuri kutaka mashtaka 14 yaliyofutwa Mahakama Kuu kurudishwa

Kesi ya Masheikh; Mahakama ya Rufaa yatupilia mbali rufaa ya Jamhuri kutaka mashtaka 14 yaliyofutwa Mahakama Kuu kurudishwa

Joined
Sep 19, 2019
Posts
43
Reaction score
383
Bismillahir Rahmanir Rahiim

SHURA YA MAIMAMU TANZANIA

MASHEIKH WAPATA USHINDI MKUBWA MAHAKAMA YA RUFAA LEO

Hukumu ya rufaa ya Jamhuri dhidi ya Masheikh imesomwa leo katika Mahakama ya Rufaa Tanzania.

Majaji watatu wa Mahakama hiyo wametupilia mbali rufaa ya upande wa Jamhuri ya kutaka mashtaka 14, dhidi ya Masheikh yaliyofutwa na Mahakama Kuu ya Tanzania yarudishwe.

Katika Mahakama hiyo leo Mawakili 9, wanaowatetea Masheikh na wanasheria 11, wa upande wa serikali walionekana wakisikiliza kwa umakini mkubwa wakati hukumu hiyo ikisomwa.

Mahakama ya rufaa imeitupa rufaa ya Jamhuri kwa hoja iliyotokana na pingamizi lililowekwa na mawakili wa masheikh kuwa Jamhuri haikuwa na haki ya kukata rufaa hukumu iliyofuta mashitaka 14 kwasababu hukumu ile haikumaliza kesi (yaani haikuwatia hatiani wala kuwaachia masheikh).

Haki ya kukata rufaa kwa Jamhuri ipo tu ikiwa hukumu imewatia hatiani au kuwaachia washitakiwa kitu ambacho hakipo katika hukumu ya mahakama kuu.

Mahakama ya rufani imesema haki ya kukata rufaa kwenye maamuzi madogo iliondolewa na mahakama ya Kikatiba na sasa Jamhuri hawana haki hiyo.

Duru za wanasheria zinasema hukumu ya leo ya mahakama ya rufaa imeleta mapinduzi makubwa katika tasnia ya sheria kwani sasa Jamhuri wameondolewa uwezo wa kukata rufaa hovyohovyo kitendo ambacho kilikuwa kinawaonea washitakiwa katika kesi za jinai na ucheleweshaji wa kesi.

Kufuatia hukumu hiyo shauri hilo sasa linarudishwa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam kuendelea kusikilizwa mashauri 11, yaliyobaki.

Aidha Shura ya Maimamu Tanzania inawapongeza Mawakili wasomi 9, wanao watetea Masheikh hao kwa kazi kubwa wanayoifanya.

Shura pia inawapongeza Watanzania wote walioitikia wito wa kuwaombea dua Masheikh hao wapate ushindi katika hukumu ya leo.

Ust. Ibrahim Z. Mkondo
Msemaji wa Shura.
0713118812
 
Sheikh hivi kwanini hawakushtakiwa kule walipotendea kosa husika yaani Zanzibar.
 
Kwahiyo wameachiwa au wanakaribia kuachiwa?
 
Mimi siuoni ushindi wowote hapo kwani mashtaka 11 bado wanayo na bado wamerudishwa kusota rumande! Aidha kama hao hawana kesi ya kujibu basi mahakama kuu ingekuwa ilifuta mashtaka yote 25. Kwa hiyo hao bado wana kesi ya kujibu ndiyo maana bado wanakula waya huko rumande ambayo ni sawa tu na kuwa jela!
 
Duru za wanasheria zinasema hukumu ya leo ya mahakama ya rufaa imeleta mapinduzi makubwa katika tasnia ya sheria kwani sasa Jamhuri wameondolewa uwezo wa kukata rufaa hovyohovyo kitendo ambacho kilikuwa kinawaonea washitakiwa katika kesi za jinai na ucheleweshaji wa kesi.
 
Hata wakiachiwa msoto wamekula. Miaka 8 sio mchezo.

Wadai fidia kila mtu bilioni.
 
Hiyo ndio hoja iliyo tumika Mahakama Kuu kufuta mashitaka hayo 14,kwamba walipaswa kushitakuwa huko huko Zanzibar kwa sababu Mahakama Kuu ya Zanzibar inauwezo Sawa Sawa na Mahakama Kuu Tanzania kwa mujibu wa Katiba na Sheria.

Sheikh hivi kwann hawakushtakiwa kule walipotendea kosa husika yaan zanzibar
 
Mabibi na mabwana hizi ni zama mpya za awamu ya Sita. Nothing more nothing less:

Habari hii inajieleza wazi. Ni suala la muda tu mabwana hawa kurejea uraiani.

=====

Dar es Salaam. Viongozi wa Jumuiya za Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar (JUMIKI), Sheik Farid Hadi Ahmed na wenzake 35 wanaokabiliwa kesi ya ugaidi wameigaragaza tena serikali mahakamani, baada ya kushinda rufaa ya Serikali iliyokuwa ikipinga uamuzi wa Mahakama Kuu kuwafutia mashtaka 14 kati ya 25 yaliyokuwa yakiwakabili.

Hatua hiyo inatokana na hukumu ya Mahakama ya Rufani kutupilia mbali rufaa ya Serikali ikisema kuwa mamlaka ya DPP kukata rufaa kwa uamuzi wa Mahakama Kuu na mahakama za chini zenye mamlaka ya ziada kutekeleza mamlaka yake una mipaka isipokuwa kwa kupinga adhabu au washtakiwa kuachiwa huru.

April 23, 2021, Mahakama Kuu iliwafutia mashtaka 14 baada ya kukubaliana na hoja za mawakili wao, Daimu Halfani, Juma Nassoro, Jeremiah Mtobesya na Abubakar Salum, kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza mashtaka hayo kwa kuwa makosa wanayotuhumiwa yanadaiwa kutendeka Zanzibar.

Serikali kupitia kwa DPP ilikata rufaa Mahakama ya Rufani kuupinga lakini wakati wa usikilizwaji wa rufaa hiyo mawakili wa washtakiwa hao waiibua pingamizi dhidi ya rufaa hiyo ya Serikali.

Pamoja na mambo mengine walikuwa wakidai kuwa DPP hana mamlaka tena ya kukata rufaa chini ya kifungu cha 6 cha Sheria ya Mamlaka ya Rufani.

Walidai kuwa kifungu hicho kilishaondolewa na Mahakama ilipotamka kuwa kinakinzana na Ibara ya 13 (1) na (2) na ya 6(a) za Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, katika kesi namba 27 la mwaka 2018, Joseph Steven Gwaza dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Akijibu pingamizi hilo, DPP alidai kuwa uamuzi huo wa mahakama katika kesi hiyo ya Gwaza ulihusu uamuzi mdogo usiomaliza shauri (interlocutory orders) na kwamba uamuzi huo unaopingwa wa kuwaondolewa mashtaka hayo unahitimisha mashtaka hayo ya jinai.

Hata hivyo, Mahakama ya Rufani katika hukumu yake iliyotolewa jana jopo la majaji watatu walioisikiliza rufaa hiyo lililoongozwa na Jaji Stella Mugasha, akishirikiana na Shaban Lila na Winfrida Korosso, ilikubaliana na hoja za pingamizi la mawakili wa Uamsho na kuitupilia mbali rufaa hiyo ya Serikali.

Mwananchi
 
Back
Top Bottom