Kesi ya 'mauaji ya Asimwe' yasogezwa mbele Padri akapimwe Akili kwanza

Kesi ya 'mauaji ya Asimwe' yasogezwa mbele Padri akapimwe Akili kwanza

Mtoa Taarifa

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2024
Posts
213
Reaction score
671
Kesi ya mauaji ya Mtoto Asimwe Novart aliyekuwa na ualbino ambaye alichukuliwa nyumbani kwao Kamachumu May 30,2024 na June 17,2024 mwili wake kukutwa kwenye kalavati akiwa ameuawa na kukatwa baadhi ya viungo vyake, imesogezwa mbele kupisha uchunguzi Mtuhumiwa wa kwanza Padri Elipidius Rwegoshora ambaye Mahakama imeamuru apelekwe Taasisi ya Isanga kwa ajili ya kupimwa akili.

Washitakiwa tisa wa kesi hiyo leo October 25 wamefikishwa Mahakama Kuu kanda ya Bukoba kwa mara ya kwanza kwa ajili ya kusomewa mashitaka yao na maelezo ya awali baada ya mwenendo kabidhi kukamilika.

Baada ya kufikishwa mbele ya Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Bukoba Emmanuel Ngigwana, Wakili Msomi Projestus Mulokozi aliyeteuliwa na Serikali kwa ajili ya kuwatetea Watuhumiwa akisaidiana na Mawakili wengine wawili ameiomba Mahakama kusitisha kwa muda kuwasomea mashtaka yao huku akiiomba itoe kibali kwa mujibu wa sheria dhidi ya Mtuhumiwa namba moja Padri Elpidius Rwegoshora kwenda kufanyiwa uchunguzi kwani wakati wanaongea nae wameona kama ana changamoto ya akili.

Hoja hiyo imeungwa mkono na Mawakili wenzake wa upande wa utetezi na Jamhuri ndipo Jaji Emmanuel akaanza kumuuliza maswali mbalimbali Mtuhumiwa huyo “unajua kwa nini upo Mahakamani?” akajibu “niliambiwa na RCO kuwa nimeua Mtoto” akamuuliza tena “tangu umezaliwa uliwahi kuwa na changamoto yoyote ya kiafya upande wa akili na ukapelekwa Hospitali?” akajibu “huaga nina tatizo la kusahau na nilisimamishwa kazi eti maneno yangu sio mazuri”.

Baada ya maelezo hayo Jaji amesema Mahakama inaona hawawezi kuendelea na Watuhumiwa hao wengine nane badala yake ametoa siku 42 kwa Rwegoshora kupelekwa Isanga kwa ajili ya uchunguzi.

Washtakiwa hao tisa kwenye kesi namba 25513 ya mwaka 2024 ni Elipidius Rwegoshora ambaye ni Padri, Novat Venant ambaye ni Baba wa Mtoto Asimwe, Nurdin Ahmada, Ramadhan Selestine, Rwenyagira Alphonce, Dastan Buchard, Faswiu Athuman, Gozibert Arikad na Dezdery Everigist ambapo nane wamerudishwa rumande mpaka December 11 mwaka huu huku Elipidius Rwegoshora akipelekwa Isanga.
 
Nimeambiwa na rco umeua mtoto mdogo! dah kuna changamoto ya akili
 
Back
Top Bottom