Jana dunia nzima ilifaidi kesi ya Mbowe na hata Jaji alisema ana taarifa kwamba proceedings za kesi hiyo zinataarifiwa mitandaoni.
Tulifaidi RPC wa Kinondoni alivyhojiwa na Advocate Kibatala hadi akaomba kwenda kukojoa.
Jioni watu wakanusa mkakati wa kukatazwa kuingia na simu, siyo Mahakama, wala si sheria, bali askari.
Dakika hizi tunavyoongea ni kweli wanautekeleza, kesi imekaribia kuanza lakini wamezuia wenye simu wasiingie nazo hivyo taarifa zidhibitiwe.
IGP alisema wana ushahidi mzito sasa kwanini wasiuelezee watu live kwenye kesi hii ambayo ni open court.
Sasa watu wa upande wa Mbowe wamekubaliana kwamba ikibidi wawatoe Mawakili wao kesi isiendelee hadi Mahakama iseme utaratibu wa Kisheria wa huu mkakati uliopangwa na polisi.
Katika hili nawakumbusha jambo moja. Mwaka 1983 akina Zacharria Hans Pope walitaka kuipindua serikali, wakakamatwa kwa kosa la uhaini.
Kesi ile ilianza kusikilizwa mwaka 1985 na gazeti la UHURU lilikuwa linaandika kila mahojiano.
Watu walifaidi uhondo kila siku. Kuna wakili wa aliyewatetea wahaini aliitwa Murtaza Lakha alipata umaarufu kuwapelekesha Serikali kama Kibatala alivyompelekesha RPC jana.
Imagine Lakha alimuuliza wakili wa serikali kuhusu tetesi kwamba mama yake Rais Julius Nyerere alikuwa mchawi hivyo alisababisha mwanaye asipinduliwe.
Kama mkuu wa nchi alitajwa hivyo kwenye kesi na ikaendelea kuandikwa magazetini iweje mtu mdogo sana kama RPC au IGP tusione anavyokomosha au kukomeshwa Mahakamani.
Hivyo tusubiri tuone nini kitaendelea, macho yote mahakamani.
Mbowe ni gaidi au siyo gaidi
UPDATE: