Kesho tutakuwapo kukipokea kile kielelezo kisichojulikana kilivyomfikia Jumanne mahakamani tokea alipomwachia Inspector Swilla.
Pamoja na kuwa kina kurasa 2 na ni ukurasa wa kwanza pekee ulio na sahihi, mchumi wa maneno aliyedhamiria anaweza kutatizika vipi hata kwenye hali tata kama hizo?
Kwamba kunasomeka Halifan, kuwa kuna majina na saini zisizokuwapo, karatasi batili ya usajili imetumika, sheria fyongo imenukuriwa kukihusisha, nk, yote yakiwa yalivyo.
Kwani akisema hakuna athari kwa mshitakiwa na kwamba kwa maoni yake nyie mtajiju, si ndiyo basi?
Akikomelea kabisa na "ninatoa AMRI" si ndiyo itakuwa kwishney?
Tatizo la kisiasa halionekani kuwa na suluhu kwenye mahakama hii.
Yote tisa, kila kona ya nchi bila kupasahau chamwino na magogoni, mdundo ni ule ule. Watu hawaridhiki na kesi hii pamoja vikorombwezo vyake ukiwamo mwenendo wake.
Sasa iko na jina jipya. Wanaiita "jumba bovu."
Kunyoa au kusuka, hiyo sasa ni shauri yake.