Kesi ya Ugaidi inayomkabili Mbowe na Wenzake watatu inaendelea tena leo , ambapo Shahidi wa tatu ambaye anajulikana kama Konstebo Msemwa ataendelea kutoa Ushahidi wake ,
Tukumbuke kwamba mashahidi wa Jamhuri zaidi ya 20 ni askari Polisi
===
Jaji ameingia..
Watu wanasimama,
Kesi inatajwa, watu wanaketi..
Jaji: Wakili wa Serikali Wakili wa Serikali anatambulisha Mawakili wa Jamhuri..
Adv. Kibatala anatambulisha Jopo la mawakili wa utetezi..
Peter Kibatala
Jonathan Mndeme
Fredrick Kihwelo
Dickson Matata
John Mallya
Sisty Aloyce
Alex Masaba
Idd Msawanga
Gaston Garubindi
Evaresta Kisanga
Hadija Aron
Faraj Mangula
Maria Mushi
George Masoud
Michael Lugina
Jaji: nimeona mawakili wa utetezi wapo upande huu, Je mpo sawa?
Wakili wa Serikali: Tupo sawa
Wakili Peter Kibatala: Tupo sawa
Jaji: Wakili Kidando wakili wa serikali: shauri limekuja kwa ajili ya kusikiliza na mpaka sasa tumeshaleta mashahidi 3 kati ya 7, na tunaomba hairisho mpaka Jumatatu.. tunaomba kupata muda wa kupitia ushahidi uliowasilishwa
Wakili wa serikali: tunaomba kuondoa mashahidi wengine waliobakia kwa dhumuni la kesi ndogo. tubakie na hao hao watatu Wakili wa Serikali anakaa chini.. Jaji: kuna lolote upande wa utetezi? Jaji anaendelea kuandika.
Kibatala: Hakuna mheshimiwa Jaji.. Jaji anaendelea kuandika..
Jaji: Shauri hili dogo kwa upande wa Jamhuri limefungwa, Nitamsikiliza wakili John Mallya...
Wakili Mallya: Mshtakiwa wa pili atajitetea mwenyewe na mashahidi wengine watatu pamoja na yeye watakuwa jumla wanne
Jaji: Kuna kingine?
Mallya: Mheshimiwa ni hayo
Jaji: Mpo tayari kuanza utetezi hata sasa? au Mngehitaji muda wa kujiandaa?
Mallya: tupo tayari Jaji anaandika. Mahakama kimya, Nje mvua inapiga kidogo
Jaji: Shahidi wa kwanza wa shauri dogo la utetezi aje kwenye kizimba.
- Shahidi anaenda kizimbani anasindikizwa na askari Magereza
Jaji: tutajie majina yako kwa ukamilifu wako unaitwa nani?
Shahidi: Adam Kasekwa
Jaji: Kuna Jina limekuwa likitumika la Adamoo unalitambua?
Shahidi: Nalitambua
Jaji: Dini yako Mkristo?
Shahidi: ndiyo
Jaji: Apa
Shahidi: Naapa mbele ya mahakama hii, yote nitakayosema yatakuwa kweli tupu, Eeh! Mwenyezi Mungu nisaidie.. Jaji unaweza kutoa ushahidi wako ukiwa umesimama au umekaa, Wakili John Mallya unaweza kuendelea.
Mallya: Shahidi umetoka kuapa, unaweza kututambulisha ulipokuja mahakamani umetokea wapi?
Shahidi: nimetokea gereza la Segerea.
Mallya: Siku za nyuma ulikuwa wapi?
Shahidi: Nilikuwa askari wa JWTZ kikosi namba 72 Sangasanga Morogoro
Mallya: ni Kikosi cha namna gani?
Shahidi: zamani kikosi cha Makomandoo siku hizi kinaitwa SPECIAL FORCE
Mallya: umehudumu kwa miaka gani?
Shahidi: Miaka sita kuanzia 2012 mpaka 2018
Mallya: Kipi kilikufanya uache kazi?
Shahidi: sikuacha bali niliachishwa na wakuu wangu
Jaji: sijui mnasikia maana naona kelele za mvua zinaingilia, KILA MTU ANAYO HAKI YA KUSIKILIZA HII KESI
Jaji: Jamani Mnasikia Wote: tunasikiaaaaaa
Jaji: Kama mkiona hamsikii tunaweza ku' break kidogo, Hasa mawakili na washitakiwa muwe free tafadhali.
Mallya: Mwaka 2016 mpaka 2017 nilikuwa kwenye misheni KONGO na Kurejek salama nchini kwangu na kuendelea na kazi.. wakuu wangu wakagundua kuwa nina tatizo la BATTLE CONFUSION
Mallya: Unaweza kumueleza, Jaji Battle Confusion inakuwaje?
Shahidi: siwezi kujijua sana lakini ni hali ya Askari anaposikia milio ya mizinga na risasi kwa wingi anakuwa hafanyi vile anavyotakiwa na wakubwa wake
Mallya: Kwenye Afya ana athiri mfumo gani? Shahidi: mfumo wa akili.
Mallya: sasa umeshafukuzwa kazi baada ya Battle Confusion, Je ulikuwa unafanya shughuli gani?
Shahidi: nilikuwa nafanya biashara ya kununua maharage huko Morogoro sehemu inaitwa Nongwe na kuuza soko la Lubeho, kote Morogoro
Mallya: unamfahamu mshtakiwa namba 4?
Shahidi: simfahamu sana ila nilitakiwa nikafanye kazi ya VIP PROTECTION
Mallya: kazi ya VIP PROTECTION ni kazi unayoweza kuifanya?
Shahidi: Ndiyo Wakili wa Serikali: OBJECTION
Mallya: naondoa swali Mallya ulifanya nini?
Shahidi: nilikuwa kwenye hatua ya mazungumzo ya kazi
Mallya: yalikuwa yanahusisha nini?
Shahidi: kuhusiana na majukumu ya kazi na malipo yetu
Mallya: ilikuwa lini?
Shahidi: Mwishoni wa mwezi wa 7 mwaka 2020
Mallya: Makubaliano ya kufanya kazi na mshtakiwa wa 4 mlikuwa mnafanya wapi?
Shahidi: mara ya kwanza tulifanya Moshi
Mallya: nakupeleka tarehe 05 Mwezi 08 mwaka 2020 kilitokea nini?
Shahidi: siku hiyo nikiwa na mshtakiwa mwenzangu namba 03 Mohammed Ling'wenya sehemu inaitwa maduka, tukavamiwa na watu kama watano, walinivamia mimi kwanza wakaanza kunipiga, mshtakiwa mwenzangu akaja kuniokoa.
Shahidi: alipofika akawauliza "Mbona mnapiga huyu mtu?".. wakamuuliza wewe unamfahamu huyu, akajibu ndiyo namfahamu.. wakachukua madawa na silaha, nikawasikia wakisema ana madawa.. wakati Mimi wakiendelea kunishambulia.
Shahidi: Mshitakiwa mwenzangu akawawahi akitoa vitu mfukoni, nikasikia kwa maneno akisema huyu mmeshamuwekea madawa? akiwa anamaanisha mimi... mmemuweka madawa na silaha? Mimi natoa vitu vyangu kabisa msije mkaniweka na mimi, Wakati huo mimi wakiendelea kunishambulia.
Mallya: unaweza Kuwakumbuka watu hao ukiwa hapa Mahakamani?
Shahidi: Mahakamani nimeshawaona watu 2
Jaji: Subiri kidogo, anaendelea kuandika.
Mallya: ni nani umewaona hapa mahakamani?
Shahidi: Ramadhani Kingai na Mahita ambao nimekuja kuwafahamu majina yao hapa mahakamani
Mallya: hawa watu wawili ambao umewataja walikuwa na majukumu gani?
Shahidi: nilikuwa nawatambua kwa sura na matendo yote ya kunipiga na kuniwekea Madawa na silaha.
Jaji: Ukisema kuwekewa madawa na silaha nini kilichotokea?
Shahidi: Wakati wananipiga na wamenibana, akaingiza mkono wake kwenye suruali akasema ana madawa na mwingine akaingiza kitu nyuma ya mkanda akatoa kitu akasema ana silaha
Mallya: hili eneo ambalo tukio limetokea lilikuwa ni eneo la wazi?
Shahidi: pana maduka ya kubadilisha pesa. M-pesa na tiGoPesa na Grocery pembeni
Mallya: Wewe ulikuwa sehemu gani?
Shahidi: nilikuwa katikati upande kulia maduka na upande wa kushoto Grocery..
Mallya: Ulikuwa umekwenda kufanya nini?
Shahidi: kuagiza chakula, Nilikuwa naandaliwa nyama ya kuchoma lakini hata kulipa bado
Mallya: nini kilifuata,?
Shahidi: baada ya mwenzangu kusema natoa vitu vyangu msije kuniwekea kama mlivyo muwekea huyu, wakatukamata na wakatufunga pingu na kutuingiza kwenye gari yao..
Mallya: baada ya kuingizwa kwenye gari waliwapeleka wapi?
Shahidi: Muda wote tulikuwa tunapigwa, hatukujua tunaelekea wapi, baadae wakatufikisha kituo cha polisi
Mallya: kituo gani?
Shahidi: nilikuaa sikijui, lakini baada ya kuongea mahakamani nimegundua ni Central Moshi
Mallya: Baada ya kupelekwa Central Moshi kitu gani kilifuata?
Shahidi: walinitoa pale ndani kituoni kuna chumba cha pembeni palikuwa na jopo la watu wengi wakanivua nguo zote, nikawa ninaning'inizwa kwenye kichuma fulani mithili ya MSHIKAKI au POPO
Shahidi: nikiwa siwezi kusimama wakanitoa pingu wakanivalisha suruali na shati, wakaanza kunikokota
Jaji: umezungumzia kuvaa!
Shahidi: Ndiyo walinivalisha suruali. wakawa wananikokota kunipeleka mahabusu, baada ya kufika mahabusu wakanifunga pingu za mikono wakaniacha ndani
Mallya: jambo gani lilifuata? Shahidi: ndani ya mahabusu kuna chumba kidogo cha mlango wa nondo wakawatoa watu mule wakanifungia mimi..
Mallya: ulijua hatima ya yule mtuhumiwa mwingine?
Shahidi: sikujua hatima yake Mallya: nini kilifuata?
Shahidi: niliendelea kukaa ndani
Mallya: kuna ushahidi umetolewa kuwa mlizunguka maeneo mbalimbali Moshi na Hai
Shahidi: hapana sikutolewa kwenda popote
Shahidi: Ndani ya chumba kuna Askari alikuja kumwaga maji
Mallya: nini kiliendelea
Shahidi: kesho yake nilikuja kugundua ni kesho tayari baada ya kuona Jua
Shahidi: wakanitoa wakinilazimisha nitembee lakini nikawa nikawa siwezi Simu inaita kwa VIBRATION (mithili ya Philips)
Jaji: naomba kila Mtu aweke simu yake katika mazingira ambayo hayaathiri kazi yangu au ya shahidi, Msilazimishe niongee Jambo ambalo sitaki kuongea..
Shahidi: sikujua naenda wapi, nilitambua tu nipo kwenye gari na ikaanza kutembea
Mallya: kitu gani kiliendelea?
Shahidi: nikiwa ndani ya gari kabla haijatoka kwa muda wa nusu saa, mateso yaliendelea kwa kunichoma choma na bisibisi
Shahidi: wakawa wananiambia "Leo ndiyo mwisho wa maisha yako, na kwamba hapa tulipo unamjua nani, nikajibu simjui Mtu, wakasema basi na wewe hakuna anayejua upo na nani"
Mallya: Endelea
Shahidi: nilikuwa nimelazwa kwenye floor ya gari, siyo kwenye siti..
Shahidi: baada ya safari ya muda mrefu sana, tukafika sehemu wakanishusha kwa kunikokota vievile na tulipofika kwenye kachumba wakanitoa Jacket wakaniuliza "Unajua upo wapi hapa?" nikawaambia "hapana sifahamu" wakafunga mlango nikiwa ndani nikiwa na pingu lakini Jacket wamenitoa
Mallya: unamkumbuka aliyekuwa anakuuliza hayo?
Shahidi: namkumbuka ni Goodluck
Mallya: Jambo gani lingine lilitokea kwenye kile chumba?
Shahidi: nikiwa na pingu nikajikokota kusogea mlangoni bahati nzuri nikaona watu wengine wamefungiwa kwenye chumba kingine kidogo mule
Shahidi: nilikaa pale tarehe 7, 8 na 9 na ilipofika tarehe 9 usiku wakaja kunichukua usiku.
Mallya: umesema umekamatwa Moshi tarehe 05 je kati ya tarehe 5 Mpaka tarehe 7 kuna nini kilitokea?
Shahidi: tarehe 05 - 7 nilikamatwa Moshi na kuteswa kisha nikasafirishwa kuja TAZARA
Shahidi: tarehe 09 wakanitoa usiku, siku hiyo angalau nilikuwa na uwezo wa kutembea, Lakini wakaniambia huku tunakoenda yanaenda kukuta yaleyale ya Moshi, sasa UJIANDAE Mallya: Tarehe 09 nini KILIFUATIA?
Shahidi: Wakinitoa wakanipandisha kwemye gari, safari ikaanza..
Shahidi: haikuchukua muda kama Moshi. Siku hiyo sikuwekwa chini kama walivyonisafirisha kutoka Moshi. wakaniingiza kwenye chumba wakanifungua
Jaji: Subiri kidogo..
Jaji: unasema mlipofika wakakushusha?
Shahidi: walifikisha mpaka kwenye chumba, Kilipofunguliwa wakanitoa Jacket usoni, wakaniamuru niingie ndani
Jaji: Ndiyo
Mallya: rudi nyuma kidogo shahidi baada ya kuambiwa kuwa upo TAZARA, Ulifanya jambo lolote kuthibitisha upo TAZARA?
Shahidi: ilipofika jioni nilikuwa nasikia mlio wa honi ya TRENI,nikagundua nipo MAENEO yanayofanana na TAZARA
Mallya: sasa tayari upo sehemu nyingine umefumguliwa koti machoni
Shahidi: niligundua umeshaingia usiku, kesho yake usiku tena akaja Kingai na Goodluck wakanitoa ndani
Mallya: Taratibu Shahidi Jaji aandike
Shahidi: wakanipeleka Kwenye chumba kilichokuwa kina meza, Goodluck akawa mlangoni na Kingai akakaa mbele yangu tukawa tunatazamana
Jaji: NDIYO
Mallya: Pingu unazozungumzia ni zipi
Shahidi: pingu za chuma
Mallya: kuna wakati wowote walikutoa Pingu tangu utoke Moshi?
Shahidi: akamuamuru Goodluck anifungua mkono mmoja, wakanifungua wa kulia wakaendelea kufunga wa kushoto, wa kulia ukawa upo FREE..