Kesi ya Ramadhan Yahaya Singano (Messi) kusikilizwa leo

wakimataifa.

JF-Expert Member
Joined
Jun 7, 2015
Posts
1,625
Reaction score
558
Ile songombingo ya mchezaji yatima aitwae Singano anayedhurumiwa haki yake kwa vitisho wa viongozi wa Simba ni leo pale TFF.

Kuna habari Messi alitaka kusaini mkataba miaka miwili Simba walitaka miaka mitatu Simba walipoona watamkosa wakakubali wakaandaa miaka miwili katika mkataba kulikuwa na malipo ya pango kila mwezi Messi akausoma akasaini ile karatasi ya mwisho ndio kuna sahihi ya pande zote mbili simba wakamwambia hizi saini zimekosewa saini hii nyingine akasaini hiyo karatasi ya pili aliosaini wakaiweka kwenye mkataba wa miaka 3.Na malipo ya pango hajalipwa akadai akaambiwa mzawa halipiwagi hela za pango.

Sasa nawambia TFF japo mmesema tusizungumzie suala hili sisi tumesema na msipoamua vizuri tutawaomba FBA.

Maana tumewachoka na mambo yenu

Uongozi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) leo umekutana na Uongozi wa klabu ya Simba SC ukiwakilishwa na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Collin Frisch na mchezaji Ramadhani Yahya Singano akiandamana na Uongozi wa Chama cha Wacheaji wa Mpira wa Miguu (SPUTANZA). Kikao hiki kiliitishwa na TFF kujadili utata wa kimtakabta kati ya mchezaji na klabu ya Simba.

Katika kikao cha leo pande zote zimeeleza kutambua utata ulio ndani ya mikataba iliyokuwepo ambayo kimsingi iliingiwa kabla ya uongozi wa sasa wa Simba SC.

Kwa pamoja pande hizo mbili zimekubaliana kuanza mazungumzo ya makubaliano mapya na hatimaye mkataba mpya utakaoanza katika msimu mpya wa 2015/16.

TFF imevitaka vilabu kushirikiana na SPUTANZA na Bodi ya Ligi katika kuweka mifumo mizuri ya uingiaji mikataba. TFF inao mkataba mama (template) ambao vilabu vyote na wachezaji wanatakiwa waufuate wakati wanaandaa mikataba yao (individual contracts between players and clubs). Aidha TFF imewataka wachezaji kuelewa mikataba kabla ya kutia sahihi.

TFF itazidi kuboresha mfumo wa usajili wa wachezaji na mikataba ili kuweka mazingira sawia kati ya pande zote mbili (Wachezaji na vilabu)
Makubaliano yamefanyika leo tarehe 9 Juni 2015 na kusainiwa na:-
  • Collin Frisch - Simba SC
  • Ramadhan Singano - Mchezaji
  • Mussa M. Kissoky - SPUTANZA
  • Mwesigwa J. Selestine - Katibu Mkuu - TFF
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
 
Jamaaaaan! Dhambi!
Nampenda kweli huyo dogo!
Mungu amsaidie apate haki zake!
 
Hiyo ipo kisheria zaidi. Atafute mwanasheria labda anaweza kumshari zaidi nn cha kufanya
 
ile songombingo ya mchezaji yatima aitwae singano anayedhurumiwa haki yake kwa vitisho wa viongozi wa simba ni leo pale tff.
kuna habari mesi alitaka kusaini mkataba miaka miwili simba walitaka miaka mitatu simba walipoona watamkosa wakakubali wakaandaa miaka miwili katika mkataba kulikuwa na malipo ya pango kila mwezi mesi akausoma akasaini ile karatasi ya mwisho ndio kuna sahihi ya pande zote mbili simba wakamwambia hizi saini zimekosewa saini hii nyingine akasaini hiyo karatasi ya pili aliosaini wakaiweka kwenye mkataba wa miaka 3.na malipo ya pango hajalipwa akadai akaambiwa mzawa halipiwagi hela za pango.

sasa nawambia tff japo mmesema tusizungumzie suala hili sisi tumesema na msipoamua vizuri tutawaomba FBA.

maana tumewachoka na mambo yenu

= anayedhulumiwa
 
binafsi nimechoshwa na hii skendo TFF fanyeni kweli kujua tatizo .ila jamani acheni ushabiki hivi yatima ni nani kwa mujibu wa vitabu vya dini?au tunanogesha stori? usiwalumu ns kuwasema vibaya wenzio kama una ushahidi ndio maana wanaenda kutafuta nani ana haki hivi akigundulika mess ndio ana tatizo utasema yatima akitaka kudhurumu?subir yatoke maamuzi ndipo unange kumuona mtu anaswali sio maana ni muadirifu cha msingi TFF wawe huru kwenyemaamuzi yasijitokeze maruweruwe(SIMBA DAMU)
 
Kwa utetezi huu wa messi eti aliambiwa kusaini tena saini zimekosewa,atakuwa kashindwa kesi kabla haijaanzwa.!!
 
ile songombingo ya mchezaji yatima aitwae singano anayedhurumiwa haki yake kwa vitisho wa viongozi wa simba ni leo pale tff.
kuna habari mesi alitaka kusaini mkataba miaka miwili simba walitaka miaka mitatu simba walipoona watamkosa wakakubali wakaandaa miaka miwili katika mkataba kulikuwa na malipo ya pango kila mwezi mesi akausoma akasaini ile karatasi ya mwisho ndio kuna sahihi ya pande zote mbili simba wakamwambia hizi saini zimekosewa saini hii nyingine akasaini hiyo karatasi ya pili aliosaini wakaiweka kwenye mkataba wa miaka 3.na malipo ya pango hajalipwa akadai akaambiwa mzawa halipiwagi hela za pango.

sasa nawambia tff japo mmesema tusizungumzie suala hili sisi tumesema na msipoamua vizuri tutawaomba FBA.

maana tumewachoka na mambo yenu

Na Leo Ndiyo Atajua Kuwa Simba Ni MAFIA WALIOTUKUKA Na Kitakachotokea Leo Nadhani Kitakuwa Ni Fundisho Kwa Wachezaji Wote Wenye VIHEREHERE. Tukishamaliza Leo Tunasitisha Sasa Rasmi Ule Mpango Wa Kumuuza Uholanzi Na Afrika Ya Kusini Japo Azam Na Yanga Wanamtaka Kwa UDI Na UVUMBA Na Kitakachofuatia Ni Kumkalisha Benchi Msimu Ujao Wote Huku Tukimpiga Miba Ya Uhakika Kama Tulivyowafanyia Wachezaji Baadhi Waliopita Ambao Sasa Wamekuwa Ni Historia. Mfano Mdogo Tu Betram Mombeki Ameondoka Simba Kwa Kashfa Ila Sasa Kila Akaapo Anasikia Tu Miguu Inawaka Moto Na Kaachana Rasmi Na Mpira Na Amerudi Kwao Mwanza Kufuga Na Kuvua Samaki. Tunaendeleza Urithi Tulioachiwa Na Mzee Wetu Marehemu Bamchawi. Chezeeni Kote ILA Siyo Kwa MNYAMA! Kafara Lililopigwa Kwa Wale Ndugu Zetu Si Mliliona Na Kusikia Matokeo Yake? Unawasikia Tena Leo? Hiyo Ndiyo Simba Sports Club.
 
Kumbe Na Wewe Mpaka Huku Michezoni Huwa Unatimba?

Mimi ni mdau wa michezo, enzi hizo ni msichana ambae miaka ya early 70s nilijifundisha karate YWCA Dar. Na ni msichana pekee niliyekuwa nafanya mazoezi ya boxing Arnatoglou hall. Na nimeshacheza sana netball enzi hizo viwanja vya Jangwani Girls. Canada nimecheza sana football kama mazoezi, ujanani, nilikuwa nikienda na Gozi langu akienda kufanya mazoezi nami ikanijia hamu ya mazoezi nikawa nafanya nao mazoezi. Mpira ni raha sana.

Gozi langu limecheza sana mpira, mpaka sasa na uzee wake huwa anaenda kufanya mazoezi ya mpira kila linapopata nafasi, tena utashangaa anafanya mazoezi na vijana.

Michezo ni jadi yangu.
 
kinachonikera ni kuwa yamkini tukaua kipaji kikubwa cha huyu dogo kwa sababu ya mivutano ilo jaa sifa za kishamba.maana mpira unataka utulivu wa akili.sasa misuko suko kwa mtoto huyu inaeza kumshushia ari.na ikumbukwe soka ndo maisha ya huyo mtoto.simba acheni sifa za kitoto nchukulieni huyo km mwanenu
 
Mimi SIMBA damu ila kwa ushenzi wanaomfanyia Singano inaonesha ni namna gani wamekosa utu!
 
Na Leo Ndiyo Atajua Kuwa Simba Ni MAFIA WALIOTUKUKA Na Kitakachotokea Leo Nadhani Kitakuwa Ni Fundisho Kwa Wachezaji Wote Wenye VIHEREHERE. Tukishamaliza Leo Tunasitisha Sasa Rasmi Ule Mpango Wa Kumuuza Uholanzi Na Afrika Ya Kusini Japo Azam Na Yanga Wanamtaka Kwa UDI Na UVUMBA Na Kitakachofuatia Ni Kumkalisha Benchi Msimu Ujao Wote Huku Tukimpiga Miba Ya Uhakika Kama Tulivyowafanyia Wachezaji Baadhi Waliopita Ambao Sasa Wamekuwa Ni Historia. Mfano Mdogo Tu Betram Mombeki Ameondoka Simba Kwa Kashfa Ila Sasa Kila Akaapo Anasikia Tu Miguu Inawaka Moto Na Kaachana Rasmi Na Mpira Na Amerudi Kwao Mwanza Kufuga Na Kuvua Samaki. Tunaendeleza Urithi Tulioachiwa Na Mzee Wetu Marehemu Bamchawi. Chezeeni Kote ILA Siyo Kwa MNYAMA! Kafara Lililopigwa Kwa Wale Ndugu Zetu Si Mliliona Na Kusikia Matokeo Yake? Unawasikia Tena Leo? Hiyo Ndiyo Simba Sports Club.

haaaaaa!!.....kumbe kweli eeh.!!
 
Kwa utetezi huu wa messi eti aliambiwa kusaini tena saini zimekosewa,atakuwa kashindwa kesi kabla haijaanzwa.!!

mesi kashinda kesi lakini mikataba yote imevunjwa.
 
Back
Top Bottom