Kesi ya Sheikh Ponda yatikisa;Afikishwa mahakamani saa 11 alfajiri

Kesi ya Sheikh Ponda yatikisa;Afikishwa mahakamani saa 11 alfajiri

nngu007

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2010
Posts
15,860
Reaction score
5,801
[h=2][/h]IJUMAA, NOVEMBA 02, 2012 11:19 NA KULWA MZEE, DAR ES SALAAM

*Afikishwa mahakamani saa 11 alfajiri
*Mahakama yazingirwa na farasi, mbwa
*Mashine za usalama zafungwa mahakamani

AMINI usiamini, jana Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, ilikuwa na ulinzi mkali usiokuwa wa kawaida. Ulinzi huo uliimarishwa wakati Katibu wa Jumuiya za Kiislamu, Sheikh Issa Ponda, alipokuwa akifikishwa mahakamani hapo, kujibu kesi ya uchochezi inayomkabili.

Pamoja na mambo mengine, ulinzi huo uliimarishwa ili kuwadhibiti baadhi ya Waislamu, ambao ni wafuasi wa Sheikh Ponda waliokuwa wamepanga kuvamia mahakamani hapo, ili kushinikiza Sheikh Ponda apewe dhamana.

Katika shauri hilo, Sheikh Ponda anashitakiwa pamoja na wenzake 49 mbele ya Hakimu Mkazi, Victoria Nongwa.

Katika ulinzi huo, taarifa zinasema kwamba, juzi saa 12 jioni, askari polisi walifika mahakamani hapo na kufunga kamera za CCTV, ambazo ziliunganishwa kutoka jengo la Raha Tower lililopo jirani na Mahakama hiyo ya Kisutu.

Baada ya hatua hiyo iliyolenga kuimarisha hali ya usalama, wakati Sheikh Ponda atakapofikishwa mahakamani hapo, jana alfajiri polisi walifika mahakamani hapo, kwa ajili ya kurekebisha mitambo yao kisha wakafunga lango la kuingia mahakamani, ili kuratibu watu watakaokuwa wakiingia mahakamani hapo jana.

Kwa kawaida, lango la kuingia mahakamani hapo huwa halifungwi, lakini kutokana na uwepo wa taarifa za baadhi ya Waislamu kufika kwa wingi mahakamani hapo, lililazimika kufungwa.

Pamoja na hayo, kila aliyekuwa akiingia mahakamani hapo jana, alikuwa akikaguliwa kupitia mashine maalum za usalama, ikiwa ni pamoja na kuulizwa maswali ni kwa nini anafika mahakamani hapo.

Kutokana na utaratibu huo mpya, wananchi waliokuwa wakifika kwa ajili ya kusikiliza kesi ya Sheikh Ponda, walikuwa wakirudishwa getini huku na waliofika kwa ajili ya kesi nyingine, walikuwa wakipekuliwa na kuruhusiwa kuingia mahakamani.

Wakati hali ikiwa hivyo, ndani na nje ya jengo la mahakama, kulikuwa na askari wengi ambao hawajawahi kuonekana.

Askari wawili walikuwa wakitumia farasi kuzunguka uzio wa mahakama, kwa ajili ya kuimarisha usalama pamoja na kuwatawanya waumini wa Kiislamu waliokuwa wamezuiwa kuingia katika mahakama hiyo.

Kikosi cha mbwa nacho hakikubaki nyuma, kwani kulikuwa na mbwa wanane, walikuwa wakionekana kuhaha mahakamani hapo, ili kuhakikisha kunakuwa na usalama wa kutosha.

Kulikuwa na askari wengi waliokuwa wamezingira maeneo ya mahakama na walikuwa wameshika bunduki, huku askari magereza kutoka kikosi maalum nao kila mmoja akiwa katika eneo lake kwa ajili ya kulinda usalama.

Mmoja wa askari aliyekuwa akiongoza farasi aliiambia MTANZANIA, kwamba, farasi mmoja alikuwa akiitwa Sai na mwingine alikuwa akiitwa Salama ambaye ni mama yake Sai.

Pamoja na wingi wa askari polisi, magereza na maofisa wa usalama wa taifa, bado wananchi waliofika kwa ajili ya kesi hiyo, waligoma kutawanyika hali iliyosababisha baadhi ya askari wenye silaha, kukasirika na kutaka kuwatimua kwa kufyatua risasi.

Baada ya wananchi kugoma kutawanyika, askari walilazimika kupanda juu ya magari na kuanza kuwatangazia wananchi, kwamba watawanyike kwa amani, lakini matangazo hayo hayakusaidia hadi walipoamua kuwafuata na kuwataka watawanyike.

Pamoja na wananchi hao kutakiwa watawanyike, bado walikuwa wakilalamika kwa kusema takbir kila wakati.

Katika shauri hilo, washitakiwa 50 wanaokabiliwa na kesi hiyo na walifikishwa mahakamani kwa mabasi makubwa matatu ya magereza yenye namba za usajili STK 9159, 9160, 9161, huku wakiwa na gari la maji ya kuwasha namba PT 0886 na magari mengine ya polisi yenye namba za usajili, PT 2066, STK 4480.

Mengine ni STK 4256, STK 0890, PT 1523 na PT 2093 yote yakiwa na askari wa kutosha, kwa ajili ya kuhakikisha usalama unakuwepo.

Washitakiwa waliingia mahakamani na kesi yao ilianza kusikilizwa saa mbili asubuhi, ambapo Mwendesha Mashitaka wa Serikali, Tumaini Kweka alieleza kesi ilipofikia.

“Mheshimiwa washitakiwa wote wako mahakamani, kesi inakuja kwa ajili ya kutajwa, upelelezi umekamilika, tunaomba tarehe ya kuwasomea washitakiwa maelezo ya awali,”alidai Kweka.

Kweka alipomaliza kusema hayo mshitakiwa namba 50, Juma Salehe, alianguka kutoka kwenye benchi na kupoteza fahamu. Hata hivyo aliendelea kuwa katika hali hiyo hadi kesi ilipomalizika.

Wakili anayewatetea washitakiwa hao, Juma Nassoro aliomba mahakama iruhusu dhamana kwani washitakiwa walipofikishwa kwa mara ya kwanza na kusomewa mashitaka mbele ya Hakimu Stuwart Sanga, hawakupewa masharti ya dhamana kwa sababu Hakimu Nongwa hakuwapo.

“Ni kweli awali masharti hayakuwekwa, niliona hoja zenu, kuanzia mshitakiwa wa pili hadi wa 50 mashtaka yao yanadhamana isipokuwa Ponda hataweza kupata dhamana, kwa sababu DPP aliwasilisha hati ya kuzuia dhamana chini ya kifungu cha sheria namba 148(4) cha sheria ya makosa ya jinai.

“Kifungu hicho kinaizuia mahakama kutoa dhamana kwa mshitakiwa, hivyo ataendelea kuwepo rumande hadi DPP atakapowasilisha hati nyingine ya kuruhusu dhamana,”alisema Nongwa.

Baada ya kusema hayo, Nongwa aliahirisha kesi hadi Novemba 15 mwaka huu, kwa ajili ya washitakiwa kusomewa maelezo ya awali.

Katika kesi hii, washitakiwa wote kwa pamoja wanadaiwa kwamba, Oktoba 12 mwaka huu, maeneo ya Chang’ombe Markaz, Dar es Salaam, walikula njama ya kutenda kosa, waliingia kwa jinai, walivamia ardhi ambayo ni kiwanja mali ya Agritanza Limited kwa nia ya kujimilikisha.

Wanadaiwa kati ya Oktoba 12 na 16 mwaka huu, walijimilikisha kiwanja hicho kwa lazima katika hali ya uvunjifu wa amani na wanadaiwa kuiba vifaa mbalimbali vya ujenzi vikiwa na thamani ya Sh milioni 59 mali ya Agritanza Limited.

“Shtaka la tano linamkabili mshitakiwa wa kwanza, Ponda Issa Ponda, unadaiwa kati ya Oktoba 10 na 16 mwaka huu, Chang’ombe Markaz, uliwashawishi wafuasi wako kutenda makosa,” alidai Kweka.

 
Hii ni kwa wasiomjua Ponda na kujiona wao ndio wasemaji wa Waislam.. ametupigania sana huyu mtu
 
Lissu ameingia hili chaka pasipo kujua ndani ndani ya chaka kuna nini.

Kwa asili ya dini ya islam Tanzania imegawanyika katika makundi mawuli makuu. Kundi watii kwa serikali na kundi wapinga serikali.

Hivyo Tundu ingetakiwa afanye uchunguzi kwanza kwamba kundi la shekh Ponda ni kundi la aiana gani na lina wafuasi kiasi gani. Vinginevyo angetakiwa awe neutral asiegamie kundi lolota. Kwa kutoegamia kundi lolote angevuna kura toka makundi yote. Lakini kwa kuegamia kundi fulani (la shekh Ponda) inampelekea aungwe mkono na upande m1 tu wa waislam.
 
Back
Top Bottom