Kesi ya TID na Ya Cheka

Kesi ya TID na Ya Cheka

Amavubi

JF-Expert Member
Joined
Dec 9, 2010
Posts
30,156
Reaction score
13,258
Je hawa si walifanya kosa moja? (kupiga) mbona Cheka kala mvua 3 na TID alikua moja tu?
 
Unajua hukumu inategemea na utetezi. Kwanza Cheka alikana mashtaka. Angeyakubali angepunguziwa hukumu. Pili alipopewa nafasi ya kujitetea mbele ya Pilato inasemekana alizoza mbovu, Kwa hiyo mahakama ikakosa sababu ya kumuhurumia na kumpunguzia adhabu!
 
Usedcountrynewpipo, Nani alikuambia ukikubali kosa ndio unapunguziwa adhabu maana hapo ndio umedhihirisha pasipo shaka kwamba wewe ndio umetenda kosa, mkuu ukipelekwa mahakamani hata kama ulimpiga mtu siku zote ni kukataa ili anaeshitaki athibitishe mahakamani kwa kuwa kinachoangaliwa ni nini chanzo cha kurushwa ngumi na mazingira ya tukio zima.

Unless kama ulikuwa unamaanisha aoneshe kujutia kile alichofanya maana alipopewa nafasi ya kujitetea kabla ya hukumu kutolewa alisema mahakama iamue vile inavyoona (which means yupo tayari kwa lolote hakuna kama zile za wengine nina mke na watoto 9 wote wananitegemea huwa zina add value kwa mtuhumiwa kwa makosa design hii.
 
Last edited by a moderator:
Cheka simwonei huruma kufungwa. Alikuwa na muda wa kutosha kusuruhisha kesi hii nje ya mahakama tangu 7/2014
Amesubiri hadi sasa.

Hiviiii alishindwa kumlipa fidia huko huko.

Alidhani serikali itamwonea huruma kwa kuwa ni bondia mzuri na anaiwakilisha nchi....eti eeeee.
 
Je hawa si walifanya kosa moja? (kupiga) mbona Cheka kala mvua 3 na TID alikua moja tu?

Cheka ni bondia,proffessional boxer,kwaiyo kwa ujuzi wake huo wa ngumi,ukimpiga mtu nje ya ulingo,unakuwa kama umempiga mtu kwa kutumia silaha,lazima adhabu iwe kali kidogo,TID,hana ujuzi wowote wa boxing unaofahamika na tahasisi muhafaka
 
Cheka alijitetea kizembe kama yupo kwa mkuu wa shina vile...
 
Sheria ya Kanuni za Adhabu, Sura ya 16 (Penal Code, Cap 16) imeainisha makosa ya jinai na adhabu zake. Kuna makosa kama ya kupiga (assault), na shambulio la kudhuru mwili (body grievous harm) na makosa mengine; na makosa hayo yana adhabu tofauti.

Ifahamike pia kuwa Mtuhumiwa anapopatikana na hatia hakimu hutumia pia sheria ya kiwango cha chini cha adhabu (The Minimum Sentence Act) ili kumpunguzia Mtuhumiwa adhabu.

Adhabu za CHEKA na TID zinatofautiana kwa misingi ya makosa walioadhibiwa nayo na pia hakimu alitumia mamlaka yake ya kuhukumu kwa kiwango gani kama ambavyo sheria inavyomruhusu.
 
Sidhani kama kujitetea kuwe kwa mjumbe au kwa Mahakama kunaondoa kosa na sheria inampa mamlaka Hakimu ya kutokuzingatia utetezi wa mtuhumiwa endapo itakuwa imethibitika kwamba mtuhumiwa alitenda kosa kwa makusudi
Cheka alijitetea kizembe kama yupo kwa mkuu wa shina vile...
 
Kwa cheka naona hakimu kampa adhabu ndogo ilitakiwa alambe kama mvua 10 hivi na viboko 50 wakati anaenda na 50 akitoka 2025.
 
Kwa cheka naona hakimu kampa adhabu ndogo ilitakiwa alambe kama mvua 10 hivi na viboko 50 wakati anaenda na 50 akitoka 2025.
Minimum Senetnce ni miaka 5 mkuu asa per Penal Code
 
Akili yako imekaa kimasaburisaburi muda wote unawaza siasa tu... vp na we unatokea kwenye kile kiwanda chetu maarufu hapa tanzania?
tujitahidi kusomea sheria walau kdg ma GT
 
Kesi hii nayo ina mvuto wa kipekee hebu ona hii: Washtakiwa: Rwakatare na Rwezaura Hakimu: Katemana Wakili wa Serikali:Rweyongeza.Ushauri: Kesi ikafanyike Kaitaba
 
Kesi hii nayo ina mvuto wa kipekee hebu ona hii: Washtakiwa: Rwakatare na Rwezaura Hakimu: Katemana Wakili wa Serikali:Rweyongeza.Ushauri: Kesi ikafanyike Kaitaba
very interesting----endelea kutupa update mkuu David
 
Back
Top Bottom