Sheria ya Kanuni za Adhabu, Sura ya 16 (Penal Code, Cap 16) imeainisha makosa ya jinai na adhabu zake. Kuna makosa kama ya kupiga (assault), na shambulio la kudhuru mwili (body grievous harm) na makosa mengine; na makosa hayo yana adhabu tofauti.
Ifahamike pia kuwa Mtuhumiwa anapopatikana na hatia hakimu hutumia pia sheria ya kiwango cha chini cha adhabu (The Minimum Sentence Act) ili kumpunguzia Mtuhumiwa adhabu.
Adhabu za CHEKA na TID zinatofautiana kwa misingi ya makosa walioadhibiwa nayo na pia hakimu alitumia mamlaka yake ya kuhukumu kwa kiwango gani kama ambavyo sheria inavyomruhusu.