Kesi ya ugaidi na uhujumu uchumi inayomkabili Freeman Mbowe na wenzake kuanza kusikilizwa Ijumaa na Jaji Mustapha Siyani

Kamanda Asiyechoka

JF-Expert Member
Joined
Sep 13, 2020
Posts
3,315
Reaction score
5,058
Kesi Na.16/2021, Makosa ya Uhujumu Uchumi yenye mashtaka ya Ugaidi ndani yake inayomkabili mwenyekiti @freemanmbowetz na wenzake 3, itaanza kusikilizwa Ijumaa ya wiki hii, katika Mahakama Kuu, Division ya Uhujumu Uchumi na Rushwa. Kesi hiyo, itasikilizwa na Jaji Mustapha Siyani.

 
Ule usemi: "Kanzu mpya, Shehe yule yule", si ajabu ukawa na nafasi yake hapa.

Tumefanikiwa kumkataa Jaji, lakini mwenye Mamlaka au Wajibu wa kupanga Majaji je?

Kama atatenda haki, tutamshukuru, ila kuondoa yote haya, Katiba Mpya pekee ndio suluhisho.

Sina imani na Serikali, Bunge wala Mahakama, bali nina imani na Mungu alie juu.
 
Muhimu mshtakiwa awe na amani na jaji atimize majukumu yake kwa kufuata sheria, sio maoni yake binafsi.
 
Kanzu mpya, Shehe yule yule.

Sina imani na Serikali, Bunge wala Mahakama, bali nina imani na Mungu alie juu.
Si ulikuwa unashanbilia jana tu hapa kwamba mmepata ushindi wa awali baada ya yule jaji kujitoa?
 
Poli jipya Nyani walewale.
 
Hama nchi.
 
Ombeni ajitoe kama inaruhusiwa kukataa majaji mfululizo na mpendekeze mlie na imani nae.
 
Inapo fika mahali wananchi wana tilia shaka vyombo vya kutoa haki, kun kuwa na giza zito mbele. Hivi kweli mahakama imekubali kupakwa matope? Kisa kukinda serikali dhalimu?
Basi Mungu atakwenda kutupa haki
 

Hakuna kesi hapo, bali majizi ya kura yanaogopa katiba mpya., hivyo wanatumia mahakama zisizo huru kukomoa wanaotaka katiba mpya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…