Cute Wife
JF-Expert Member
- Nov 17, 2023
- 1,906
- 5,000
Wakuu,
Hii kesi naona mauzauza, inaenda kama haiendi inakuja kama haiji. Yaani wanafanya kusudi kabisa ili iishie juu kwa juu. Ngoja tuone nini kitajiri hiyo kesho wakati CHADEMA wakiuamua mbivu na mbichi.
=====
Kwa mara nyingine tena Mahakama ya Hakimu Mkazi Kivukoni, iliyopo Kinondoni imeshindwa kuendelea na usikilizwaji wa kesi ya jaribio la kumteka mfanyabiashara Deogratius Tarimo.
Kesi inayowakabili mjasiriamali, Fredrick Said na wenzake watano ilikuwa imepangwa leo Alhamisi, Januari 9, 2025 kwa ajili ya usikilizwaji wa awali, kwa washtakiwa wangesomewa maelezo ya awali ya kesi na kisha usikilizwaji kamili, yaani Mahakama kuanza kupokea ushahidi wa upande wa mashtaka.
Hata hivyo, mahakama hiyo haikuweza kuendelea kutokana na jalada la kesi kutokuwepo.
Mwendesha mashtaka, Wakili wa Serikali Daisy Makakala ameieleza mahakama kesi hiyo haiwezi kuendelea kwa kuwa hakuwa na jalada, huku akifafanua liliitwa Dodoma (Makao makuu ya Ofisi ya Taifa ya Mashtaka – NPS).
Pia soma: Waliomteka Tarimo (akina Benki) wamerudi uraiani dhamana yao imepita kimyakimya, kesi kuendelea Januari 9, 2025
"Shauri hili lilikuja kwa ajili ya hoja za awali lakini hatuko tayari kwa kuwa sina jalada halisi na kwa taarifa nilizonazo ni kwamba lilikuwa Dodoma lakini liko njiani linakuja. Hivyo tunaomba tupangiwe tarehe nyingine," amesema Wakili Makakala.
Hoja hiyo haikupingwa na washtakiwa na Hakimu Mkazi Mkuu, Ramadhani Rugemarila ameahirisha kesi hiyo mpaka Januari 21, 2025 kwa ajili ya kuendelea na hatua hizo.
Hii ni mara ya pili mfululizo kukwama. Mara ya kwanza ilipangwa kusikilizwa katika hatua ya awali na kisha kuendelea na ushahidi Desemba 19, 2024.