Mtoa Taarifa
JF-Expert Member
- Sep 21, 2024
- 213
- 671
Mahakama ya Hakimu Kisutu iliyopo Dar es Salaam, imeahirisha kesi inayowakabili wamiliki wa jengo la ghorofa lililoporomoka eneo la Kariakoo hadi Januari 13, 2025 kwa ajili ya kutajwa.
Kesi hiyo imeahirishwa mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi wa mahakama hiyo Godfrey Mhina baada ya Wakili wa Serikali Roida Mwakamele kuieleza mahakama kuwa upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika hivyo kuomba mahakama ipange tarahe nyingine kwa ajili ya kutajwa.
Wamiliki hao ni Leondela Mdete, Zenabu Islam (wote wakazi wa Kariakoo) na Ashour Awadh Ashour (mkazi wa llala) ambao kwa pamoja wanakabiliwa na shtaka la mauaji pasipo kukusudia.
Wamiliki hao wanatuhumiwa kushindwa kutimiza majukumu yao ipasavyo na hivyo kusababisha vifo vya watu 31 baada ya ghorofa wanalomiliki eneo Mtaa wa Mchikichi na Congo, Dar es Salaam kuporomoka Novemba 16, 2024.
Baadhi wa washtakiwa hao wapo nje kwa dhamana huku wengine wakikosa vigezo vya kupata dhamana, na kuendelea kusota rumande.