Kesi ya Wema, mahakama yafurika atinga na wapambe kibao watu wapagawa

msafwa93

JF-Expert Member
Joined
Jul 2, 2011
Posts
4,786
Reaction score
5,963


KESI ya kudaiwa kumtukana matusi ya nguoni na kumpiga vibao Meneja wa Hoteli, Goodluck Kuyumbu inayomkabili Staa wa Filamu, Wema Isaac Sepetu imeunguruma Jumatano iliyopita

katika Mahakama ya Mwanzo Kawe jijini Dar na watu kufurika pomoni, Ijumaa linakumegea kilichojiri.

Katika mahakama hiyo watu walifurika kwa lengo la kutaka kumuona Wema aliyepandishwa mbele ya Hakimu, Bernice Ikanda kusomewa mashtaka ya kudaiwa kufanya vurugu, kushambulia kwa kumpiga makofi na kumtukana Goodluck.


ATINGA NA MSAFARA
Wakati wa kuwasili mahakanai hapo, Wema aliambatana na msafara wa magari matatu, yeye akiwa katika lake la aina ya Audi Q 7, magari mengine yalikuwa ni Toyota Opa na Toyota Hiace yaliyokuwa na watu wake.




WATU WAFURIKA MAHAKAMANI
Kutokana na jamii kupenda kufuatilia matukio ya kila siku ya Wema, watu kibao walifika mahakamani hapo kusikiliza kesi hiyo.
Mara baada ya mlimbwende huyo wa mwaka 2006-07kuzama katika chumba cha mahakama, kulitokea vurugu kwa baadhi ya watu kukanyagana ili kutaka kumuona na kusikilza kesi hiyo kwa ukaribu zaidi.



AINGIZWA CHUMBA CHA MAHAKAMA

Wema aliingizwa katika chumba cha mahakama sambamba na Goodluck ambapo Hakimu Bernice alianza kumuuliza mlalamikaji kama alikuwa na mashahidi walioshuhudia tukio hilo lilivyotokea.
Goodluck alijibu kuwa anao mashahidi na kumwambia hakimu kwamba anaweza kuwaleta mbele ya mahakama hiyo.





KESI YAPIGWA KALENDA TENA
Hakimu aliamuru kesi hiyo iahirishwe hadi Agosti 20, mwaka huu na kumtaka mlalamikaji kufika na mashahidi wake.
Kuonesha kwamba watu wengi walikuwa wamefika kushuhudia kesi hiyo, walitawanyika baada ya uamuzi huo.



WEMA ANUNUA MIHOGO
Mara baada ya kutoka mahakamani na kuruhusiwa kuondoka kutokana na dhamana aliyonayo, Wema alionekana akinunua mihogo kwa ajili ya futari ya siku hiyo.

 
naona alibeba na waandishi kabisa
 
asiidharau hii kesi muulize t.i.d
 
Habari nyingine bana, zimejaa ujingaujinga tu!!! yaani huyo malaya hata akikohoa tu kwao tayar ishakuwa habari! mbona miaka ya nyuma walikuwepo mastaa wenye akili kuliko huyo mpumbav wenu, kulikuw hakuna habar za kijinga kama hizi!
 
yaan wema hana jambo dogo!! sasa watu wote wa nini hao!!
 
hahahaha da kipindi chake hicho kinapata clip.
 
Yaani kununua mihogo nayo ni habari ya kutuandikia?
 
hahaha nicheke mie, sidiria nyekundu, simu nyekundu, sketi nyekundu, viatu vyekundu kitambaa cha kichwani chekundu dah! amemechishaje?
 
Reactions: amu
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…